NMB yafutarisha Zanzibar

22:30 by Kwetuhouse Media

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza mara baada ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya NMB Tawi la Zanzibar iliyofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ni Meneja Mkuu wa Idara inayoshughulikia fedha ya NMB Bwana Waziri Banabas na kushoto yake ni Meneja wa huduma kwa wateja wa NMB Bwana Majid.
 Baadhi ya wateja na walikwa futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya NMB Tawi la Zanzibar ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
 Baadhi ya wateja na walikwa futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya NMB Tawi la Zanzibar ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

 Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar Bwana Abdulla Duchi akitoa neon la shukrani kwa wateja na wananchi walioalikwa na Uongozi wa Benki hiyo katika futari ya pamoja hapo Zanzibar Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
 Meneja Mkuu wa Idara inayoshughulikia fedha ya NMB Bwana Waziri Banabas akielezea mikakati ya Benki hiyo mara baada ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki hiyo Tawi la Zanzibar hapo Kilimani.
 Balozi Seif aliyepo kati kati kwa waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Benki ya NMB Makao Makuu Dar es salaa na Tawi la Zanzibar.

Kulia ya Balozi ni Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikha Fadhil Suleiman Soraga, Meneja Mkuu wa Idara inayoshughulikia fedha ya NMB Bwana Waziri Banabas, kushoto ya Balozi ni Meneja wa huduma kwa wateja wa NMB Bwana Majid na Mstahiki Meya wa Mji wa Zanzibar Khatib Abdulrahman Khatib.
  Balozi Seif akibadilishana mawazo na baadhi ya Viongozi wa Benki ya NMB Pamoja na Wananchi walioshiriki futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki hiyo Tawi la Zanzibar.
Balozi Seif akiagana na Baadhi ya Viongozi wa Benki ya NMB hapo Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani mara baada ya kukamilika kwa futari ya pamoja.

Picha na – OMPR – ZNZ.

0 comments:

Post a Comment