Licha ya Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon kuitaka serikali ya Burundi kuakhirisha uchaguzi
nchini humo, mwakilishi wa nchi hiyo kwenye umoja huo amesema kuwa, uchaguzi wa
bunge utafanyika katika tarehe iliyopangwa.
Albert Shingiro,
aliyasema hayo jana Ijumaa na kutangaza kuwa, uchaguzi huo utafanyika siku ya
Jumatatu ijayo huku ule wa rais ukipangwa kufanyika tarehe 15 mwezi Julai.
Shingiro amesisitiza kuwa, kuakhirishwa tena uchaguzi nchini Burundi, ni kwenda
kinyume na katiba.
Kabla ya hapo Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon alikuwa amesema kuwa, kutokana na hali ya
kutia wasi wasi ya kisiasa na kiusalama nchini humo, haitakuwa sahihi kufanyika
uchaguzi katika tarehe iliyopangwa yaani tarehe 29 ya mwezi huu. Hayo
yanaripotiwa katika hali ambayo, Alkhamis iliyopita, kulianza kampeni za urais
ambazo zitaendelea hadi tarehe 12 ya mwezi ujao.
Burundi ilitumbukia
katika machafuko tangu mwishoni mwa mwezi Aprili, baada ya chama tawala cha
CNDD-FDD kumwidhinisha Rais Pierre Nkurunziza kugombea kwa muhula wa tatu
katika uchaguzi wa rais, suala ambalo linatajwa na upande wa upinzani kuwa, ni
kinyume cha katiba na pia makubaliano yaliyofikiwa mjini Arusha, Tanzania.
Katika machafuko hayo karibu watu 80 wamekwishauawa, huku maelfu ya wengine
wakilazimika kuwa wakimbizi katika nchi jirani.
0 comments:
Post a Comment