Mimi ni Jane naishi mwenge Dar es salaam
naomba utalifuta jina la baba yangu maana sitaki liwe kwenye blog watu
watanijua na kuniangamiza maana nimeshawaangamiza wengi sana kwa UKIMWI ila
mengine yote usifute hata moja ili dunia ijue tu japokua mimi nitakufa kwa huu
ukimwi nilionao.
Nilizaliwa mkoa wa Dodoma na nilishi vizuri tu tangu utotoni na hata sikujihusisha
na ngono hadi nilipomaliza form 4 mwaka 2006 baada ya kumaliza nilikuja hapa
Dar kuishi kwa mama mdogo aliyeolewa hapa Mwenge.
Nilipata marafiki wengi tu na kuna kijana mmoja
alinitongoza kwa muda mrefu sana na siunajua vijana wengi hutumia muda mrefu
kutongoza ili msichana unadhani kwamba labda huyo anakupenda kumbe anataka tu
ngono na wadada wengi sana hudhani kufuatiliwa kwa muda mrefu na mvulana basi
huyo yuko serious kumbe hakuna lolote.
Nilimkubalia tukawa wapenzi ila nilikataa
kuhusu kufanya mapenzi maana anayekupenda kiukweli sio uongo lazima asitake
ngono kabla ya ndoa.
Kwa miezi kama 5 hadi 6 aliniambia kuhusu
kufanya mapenzi nilikataa alitumia mbinu nyingi sana kwa kunibembeleza na hata
kulia mbele yangu ili tufanye tu mara moja ila nilikataa, alisema atavumilia
hadi siku ya ndoa yetu ambapo tulipanga kuoana mwaka sept 2009.
Siku moja aliniambia twende kwenye kumbi za
starehe na mimi kwa sababu ya upagani na kumwamini pia kwa sababu nampenda
nilikubali tulienda huko na kulikua na bendi fulani maarufu ya mziki wa dansi
ilikua inatumbuiza.
Tulitafuta sehemu na kukaa na mpenzi wangu
akaagiza pombe alianza kunywa huku akinionjesha, nilikataa kwa sababu nilikua sijawahi
kunywa pombe katika maisha yangu yote, hata sijui alinishawishi vipi nilijikuta
nakunywa kidogo kidogo na kwa kuwa tulikaa pale kwa muda zaidi ya masaa 5
nadhani nikunywa kama bia 3 au 4 japokua nilikua nakunywa kidogo kidogo tu tena
kwa kunywesha na mpenzi wangu maana nikama nikua nanyweshwa kila baada kama ya
dakika 25 ndipo nakunywa mara moja na sikujuia kama nakunywa pombe ila
niliihisi tu naonja ili kumlizisha mpenzi wangu.
Ilipofika saa 10 alfajiri nilihisi usingizi na
pia nilijiona wa tofauti najua nililewa hata kama sikujua kama nimelewa maana
nakumbuka tulitoka pale huku amenishika mkono huyo mpenzi wangu. Tulikodo tax
na kuondoka na siku hiyo aliniambia twende kwake alikokua amepanga chumba maana
tulikua na usingizi sana nilikubali huku nikidhani hatuwezi kufanya mapenzi.
Tulifika salama na kuingia ndani ukweli pombe
ni kichocheo cha ngono na ningekua mimi ndio Raisi wa Tanzania ningefunga bar
zote.
Nilijikuta natamani kufanya mapenzi na huyu
mpenzi wangu hata alikua hana nia maana alijua atanichukiza sana na uhusiano
ungekufa siku hiyo lakini kwa sababu ya pombe nilimwambia siku hiyo tufanye
kidogo maana mwili wangu unataka.
Ni kweli siku hiyo kwa sababu ya pombe
nilifanya mapenzi na huyo mpenzi wangu na baadae akanipeleka nyumbani baada ya
wiki mbili maana tulikaa wiki mbili bila kuonana alikuja na kunieleza habari
ambayo sikuihitaji katika maisha yangu maana nilikua nasikia tu kwa watu
wengine lakini sio kwangu alisema ”JANE ISHI KWA MATUMAINI KUANZIA SASA”
Nilidhani utani lakini aliniambia kuwa yeye
ana UKIMWI tangu miaka mitano iliyopita na anapenda tu ngono maana hawezi
kuacha.
Nililia sana na baada ya wiki moja baadae
nikaenda kupima na kukutwa nina ugojwa ambao niliusikia tu kwa watu na chanzo
cha yote ni pombe, kupenda starehe,disko na upagani unaotusumbua wanadamu
wengi.
Nilikua na UKIMWI na kwa hasira maana mpenzi
wangu alihamia Arusha huku akisema neno moja la mwisho kwamba ”shetani amemtuma
kuwaambukiza wanadamu UKIMWI”
Sikujua, sikujua, sikujua, sikujuaaaaaaaaa, basi tu ooh YESU nihurumie mimi leo.Nilibebeshwa mzigo ambao haukunistahili mimi. Hata leo hua najiuliza kwamba nilijitunza kwa miaka 23 yote lakini pombe na huyu wakala wa shetani wamenifanyia hivi.
Baada ya kujua nina UKIMWI na hali hiyo
nikaikubali na kulikua na kundi kubwa sana la wanaume ambao walikua wamewahi
kunitongoja na niliwakataa sana kwa sababu hii niliwakubali ili nami nife na
wengi.
Nilianza kumkubali kila mmoja na kuna baba
mmoja ambaye ana wake 3 niliwahi kumtukana sana kipindi cha nyuma kila aliponitongoza
lakini wakati huu nilimkubali na hakuamini na tukafanya ngono tena bila kinga
na akaniaachia pesa laki 6 kama zawadi ya kumkubali kumbe naye hakujua kuwa
namwambukiza na hata leo hua nawahurumia tu wale wake zake ambao wana UKIMWI
uliotoka kwangu.
Kiukweli tangu may 2009 hadi 2012 nimeshatembea na wanaume zaidi 1500 maana ilifika kipindi nala na wanaume 3 kwa siku na lengo langu niwakomeshe kama mimi nilivyokomeshwa na nina uhakika kutokana na mimi wameambukizwa UKIMWI wanadamu zaidi ya 10,000 na hili tangazo la ”TUKO WANGAPI” huwa linaniliza kila siku maana hata mimi najua kabisa nilianzisha mtandao kama huo wa ngono kwa idadi kubwa sana ya watu.
Nimeokoka miezi 7 iliyopita na siku naombewa
nilikutwa na mapepo mengi sana na hata waombeaji wakashangaa. Ningejua
ningeokoka tangu nikiwa na miaka 5 lakini ndio hivyo sina jinsi wala uwezo wa
kubadirisha hali hiyo.
Na naomba kila atakayesoma ujumbe huu ajue kuanzia leo kuwa pombe ni dhambi pia kwenda disko ni dhambi,kuuza pombe ni dhambi na kila kichochoe chochote cha dhambi ni dhambi. Hadi sasa mtu yeyote hawezi kujua kama nina UKIMWI na sijui MUNGU ana mpango gani na mimi maana kwake yote yanawezekana. Nauamini uponyaji wake na sijawahi kutumia ARV hata siku moja na afya yangu iko sawa tu na huwezi hata wewe kujua kama uovu huu nimefanya mimi.
Na naomba kila atakayesoma ujumbe huu ajue kuanzia leo kuwa pombe ni dhambi pia kwenda disko ni dhambi,kuuza pombe ni dhambi na kila kichochoe chochote cha dhambi ni dhambi. Hadi sasa mtu yeyote hawezi kujua kama nina UKIMWI na sijui MUNGU ana mpango gani na mimi maana kwake yote yanawezekana. Nauamini uponyaji wake na sijawahi kutumia ARV hata siku moja na afya yangu iko sawa tu na huwezi hata wewe kujua kama uovu huu nimefanya mimi.
Ndugu zangu kama una UKIMWI nenda kanisani ukaombewe na kama una akili mpe YESU
maisha yako maana pia baada ya kifo ni hukumu. Yasalimishe maisha yako kwa YESU
na usiambukize wengine tena.
Mimi tangu niokoke sijawahi kufanya mapenzi tena na sitafanya hivyo wala
sitaolewa na mtu yeyote maana yatosha kwa uovu niliofanya na hadi sasa wapo
ninaowajua zaidi ya 15 wameshafariki na nilihudhulia misibani huku nikijua
kabisa chanzo ni mimi.
Mwisho nawashauli wababa kulidhika na wake zao na wamama pia lidhikeni na waume
zenu, vijana ambao hamjaoa wala kuolewa subiri hadi utakapooa au kuolewa na
kabla ya kuolewa au kuoa kapimeni kwanza kwani wenye UKIMWI ni wengi kuliko
unavyozani.
Fuata unachofundishwa kanisani na pia soma BIBLIA na uwe mtakatifu.
MUNGU akubariki
Ni mimi Jane, Mwenge, Dar es salaam Tanzania
0 comments:
Post a Comment