Wajumbe wa baraza
la wawakilishi kutoka Chama cha Wananchi CUF leo wametoka nje ya ukumbi wa
baraza hilo kwa kile wanachodai ukiukwaji wa sheria, ikiwemo kujaza askari
Polisi na wengine wakivaa ninja katika uwandikishaji wa Daftari la wapiga kura
linaloendelea visiwani Zanzibar.
Wakizungumza na
waandishi wa habari katika ukumbi wa Makao makuu ya chama hicho Vuga mjini
Unguja walisema kwamba wameamua kutoka kwa lengo la kupinga matokeo ambayo
yanendelea kutokea katika uandikishaji wa daftari kwa wilaya za magharbi ambayo
yanakwenda kinyume na sheria za Nchi.
Akizungumza kwa
niaba ya wawakilishi na mawaziri wa SMZ kutoka upande wa CUF Juma Duni Haji
makamo mwenyekiti wa chama hicho alisema ni jambo la kushangaza katika nchi
iliokubali demokrasia kuona askari wanavaa ninja bila ya sera zao wakiwatisha
watu wanaokwenda kujiandikisha.
“Huu jamani ni
uhuni unaingiza majambazi katika vituo vya kujiandikisha halafu unasema ni
askari wa kulinda Amani, hemu niambieni mumeona wapi mambo hayaa ispokua hapa
kwetu” alisema Haji.
Alisema tokea
uwandikishaji huo kuaza katika kisiwa cha Unguja umekuwa na vurugu kutokana na
chama cha Mapinduzi CCM kuingiza wageni na watoto wadogo kutoka nje ya jimbo
husika.
Lakini pia Juma
duni Maarufu kama Babu alisema wao wametoka barazani lakini wataendelea kuwa
mawaziri na wawakilishi mpaka mwisho wa Serikali ya awamu hii.
“Sisi ni mawaziri
na tutakuwa mawaziri mapaka Rais atakapo sema basi au muda wetu kumalizika,
sambamba na wawakilishi hadi litakapo vunjwa baraza la Wawakilishi hapo june 26
mwaka huu” alisema Haji.
Alieleza kuwa
wataendelea kuitumikia serikali lakini hawatojishuhulisha na shuhuli za baraza
hilo kwa kipindi hiki, na hawatohudhuria katika ufungaji wake ambapo Rais wa
zanzibar atalihutubia baraza hilo hapo tarehe 26 mwezi huu sambamba na
kulivunja rasmi.
Kabala ya kukimbia
shuhuli za bara hilo waziri wa Mawasiliano na Miundombinu ndie aliyesimama na
kutoa malalamiko hayo kwa spika wa baraza hilo Pandu Ameir kificho, na baadae
wote kutoka nje huku wakiacha bajeti ya wizara ya fedha ikiendelea kujadiliwa.
Mapema Naibu katibu
Mkuu wa chama hicho Nassor Ahmed Mazurui alisema ameziona kambi za Jeshi tatu
zanzibar zinatumika katika kuwapatia watu vitambulisho vya mzanzibar mkaazi
kinyume na utaratibu.
“Nimekwenda mpaka
kwenye kambi ya Chukwani, nikakaaa kwenye geti, nikaziona gari tatu namba
ninazo wanaingia na vijana ambao ni watoto wadogo na watu kutoka
Tanzania bara
kwa ajili ya kupewa vitambulisho vya Zan id” alisema Mazurui.
Alisema tayari
walishamueleza Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete juu ya Jeshi la wananchi(JWTZ)
linavyotumika katika siasa wazi wazi lakini bado hali haijabadilika kutokana na
jeshi hilo kuendelea na mchakato huo kama kawaida.
Alisema kwa
ushahidi walionao kambi ya jeshi Chukwani, mwalimu nyerere, Bububu na Dunga
iliyooko wilaya ya kati ndizo ambazo zinahifadhi vijana wa aina tofauti kwa
ajili ya kuendikishwa katika daftari la wapiga kura.
Akijibu suali juu
kushiriki uchaguzi mkuu alisema licha ya uharibifu wote unaotokea hawatosusia
uchaguzi na kujigamba kwamba gharama yoyote watashiriki.
“Hapa hapana dezo
kuwa tuwaachiee CCM wachukua Serikali hivihivi tuu tutashirikia uchaguzi kwa
vyovyote vile itakavyokua”alisema Mazurui.
Alisema chama chake
kimejipanga kushiriki uchaguzi hata kwa mazingira gani ili kiweze kuwakomboa
wananchi na dhulma ilyodumu muda mrefu.
Kufuatia wajumbe wa
CUF kutoka nje ya baraza hilo mwakilishi wa kwamtipura Hamza Hassan Juma
akichangia bajeti wizara ya fedha aliliomba baraza hilo kuongeza siku tatu, ili
aweze kupeleka hoja binafisi ya kuwataka wananchi kupiga kura ya maoni kuamua
kuwepo au kutowepo serikali ya Umoja wa Kitaifa.
“Waziri ndie
anasusia shuhuli za Serikali ndani ya baraza hili kwa kweli ni gumu na si vyema
kuendelea na Serikali ya umoja wa kitaifa kwani wezetu hawaitaki” alisema Juma.
Alisema kwa sababu mawaziri wote wametoka basi ni vyema na vyombo vya Serikali
kuvirejesha.
Tendo hilo la
kususia kikao cha baraza kinachoendelea kilionekanakana kwamba kimekasirisha
wawakilishi wa CCM waliokuwemo wakati huo na kuwafanya wote kutaka GNU ivunjwe.
Miezi miwili
iliopita akizungumza na waandishi wa habari ofisini kawake mkurugenzi wa tume
ya uchaguzi Zanzibar (ZEC)Salum kassim Ali alieleza kuwa tume hio haina
mafungamano na taasisi yoyote hile katika ufanyaji kazi wake na wamekuwa wakifanya
kazi zao kwa ustadi mkubwa licha ya chama cha CUF kupinga vikali kauli hio kwa
mujibu wa taarifa waliotoa kwa waandishi wa habari.
0 comments:
Post a Comment