Rais wa
TFF. Jamal Malinzi amemtangaza Charles Mkwasa kuwa kocha mpya wa Taifa Stars
akisaidiwa na kocha Hemed Morocco, Mkwasa ambaye ni kocha wa Yanga na Morocco
kocha wa Mafunzo watafanya kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo timu ya
taifa itakua na michezo ya kuwania kufuzu kwa CHAN na AFCON.
Malinzi
amesema uteuzi wa makocha hao wazawa umezingatia vigezo vya makocha wa timu ya
Taifa kuwa na leseni A ya ukocha kutoka CAF au zinazofanana kutoka mashiriksho
mengine duniani wanaozifanyia kazi, jambo ambalo makocha hao wazawa
wamekizi.
Kocha
Mkwasa atakua akipewa hudumu zote na masilahi (zikiwemo posho) alizokuwa
anapewa kocha aliyeondoka, pia amepewa nafasi ya kuchagua benchi lake la ufundi
la kufanya nalo kazi, hivyo nawaomba wadau wa mpira wa miguu na watanzania kwa
ujumla tuwape sapoti makocha hao wazawa” aliongeza Malinzi”
Aidha
Kamati ya utendaji ya TFF Iimemteua Alhaj Ahmed Mgoyi kuwa mratibu wa timu ya
Taifa, lengo la uteuzi huo wa Mgoyi ni kuwa kiunganishi kati ya kamati ya
Utendaji na timu ya Taifa.
Wakati
huo huo, timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 ya Tanzania,
imeingia kambini jana na kuanza mazoezi leo katika uwanja wa Karume kujiandaa
na mchezo wa kirafiki dhidi ya kombaini U15 ya mkoa wa Mbeya siku ya jumapili.
Kikosi
hicho kilicho chini ya makocha Bakari Shime na Peter Manyika kitacheza mchezo
huo kwa lengo la waalimu kupatawa fursa ya kuwaona vijana hao na kuwaongeza
wengine watakaoneka katika kikosi hicho.
U15 ni
mpango wa TFF kuandaa kikosi kizuri chenye ubora kuelekea kuwania kufuzu ka
fainali za vijana Afrika mwaka 2017 zitakazofanyika nchini Madagascar, ambapo
vijana hao watakua na umri wa miaka 16 kufikia mwakani wakati michezo ya
kuwania kufuzu itakaponza mwezi Julai, 2016.
0 comments:
Post a Comment