Kampuni ya Boti za Azam Marine Zanzibar yatowa Boti Mpya ya Kilimanjaro
V,iliowasili juzi katika bandari ya Zanzibar na inategemewa kuaza kutoa
huduma ya Usafiri kati ya Zanzibar na Dar-es-Salaam mwishoni mwa wiki
hii baada ya kukamilisha taratibu zote za kisheria na kuaza kutowa
huduma hiyo. Ikiwa katika bandari ya Zanzibar leo.Ina uwezo wa kuchukua
Abiria 550, inachukua masaa maskamu lisaa moja na nusu mpaka Dar.
Kepteni wa Boti Mpya ya Kilimanjaro V Thomas Buhatwa akizungumza na
waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya Zanzibar kuhusiana na
huduma zinazopatikana katika boti hiyo mpya na kutowa maelezo ya vyombo
vya kisasa viliomo katika boti hiwa wakati wa kuitembelea boti hiyo
ikiwa katika bandari ya Zanzibar leo mchana.
Kapteni Thomas Buhatwa akionesha mitambo ya kisasa ya boti hiyo
inayoonesha hali halisi ya bahari wakati wa safari zake akiwa katika
chumba cha makepteni katika biti hiyo wakati waandishi walipotembelea
biti hiyo mpya.
Meneja Mkuu wa Azam Marine Ndg Hussein M Said, akizungumza na Waandishi
wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibarv wakati waandishi hao
walipoitembelea Boti hiyo Mpya na kupata maelezo kutoka kwa Meneja, Boti
hiyo ikiwa katika bandari ya Zanzibar na kuelezea uina uwezo wa
kuchukua abiria 550 kwa wakati mmoja na mizigo pia amesema ina uwezo wa
kusafiri kati ya Zanzibar na Dar kwa muda wa saa moja na nusu, Amesema
inatarajiwa kutowa huduma mwishoni mwa wiki hii ikikamilisha taratibu
zote zilizobaki katika vyombo husika.
Sehemu ya VIP One ikiwa na Video katika viti vyake vyenye uwezo wa kulala wakati abiria wakiwa safarini.
Sehemu ya VIP kama inavyoonekana
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Marine Ndg Hussein M Said, akizungumza na
Mwakilishi wa kampuni ya RDM- Marine Engineer ya Australia Egn Kerry
Williams, wakiwa katika boti hiyo baada ya ukaguzi na majaribio ya Boti
hiyo yaliofanyika hadi katika visiwa vya Chumbe na kurudi baada ya
ukaguzi uliofanywa na ZAM.
0 comments:
Post a Comment