Staa wa bongo movie Jacqueline Wolper Massawe
‘Twiga wa Jangwani’. UPO? Mtoto mzuri katika tasnia ya uigizaji Bongo,
Jacqueline Wolper Massawe ‘Twiga wa Jangwani’ amesema haoni sababu ya kuukana
uanachama wa taasisi ya Wajenzi Huru (Freemason) kwani ni dini kama zilivyo
zingine na kama katiba inavyoelekeza, kila mtu anayo haki ya kujiunga na dini
au taasisi yoyote ya kuabudu kulingana na matakwa ya imani yake.
Jacqueline Wolper Massawe akiwa katika pozi.
Akichezesha taya na Amani, Wolper alisema ni kweli yuko katika kundi hilo huku
akishangaa watu kustaajabu kuona mtu yuko Freemason wakati walioanzisha dini
hiyo ni binadamu kama wengine.
“Freemason si ni
taasisi au dini kama zingine? Kuna ajabu gani mimi kuwa mwanachama? Tena nataka
nikuhahakikishie kuwa, nimekuwa muumini halisi wa Freemason kwa muda mrefu
sasa,” alisema Wolper
0 comments:
Post a Comment