Serikali
imepiga marufuku halmashauri za wilaya na manispaa nchini, kuchukua ardhi ya
wananchi bila kuwalipa fidia.
Amri hiyo
imetolewa mjini hapa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William
Lukuvi (pichani), wakati akijibu malalako ya wananchi kuhusu upatikanaji
na umiliki wa ardhi.
Lukuvi,
alisema halmashauri na manispaa nchini, zimekuwa zikichukua ardhi ya wananchi
bila makubaliano na kuwalipa fidia kwa kisingizo cha upimaji viwanja au kutoa
maeneo hayo kwa ajili ya uwekezaji.
Alisema
kitendo hicho ni dhuluma kwa wananchi na kwamba kamwe hakikubaliki.
Awali
baadhi ya wakazi hao, walimlalamikia Waziri Lukuvi wakidai kuwa wamekuwa
wakiporwa ardhi na maofisa wa halmashauri na manispaa bila maelezo.
Walidai
wanapofuatilia kwenye ofisi zao, wamekuwa wakijibiwa vibaya na wakati mwingine
kulipwa fidia kidogo ambayo haitoshi kununua kiwanja na kuwa kero kubwa
kwao na kukatisha tamaa.
Akizungumza
huku akibubujikwa na machozi mbele ya Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Ismani,
Zuhura Chavala, Mkazi wa Kijiji cha Migori, alidai maofisa ardhi wamekuwa
wakiwadhulumu baada ya kuwaponya ardhi yao.
Zuhura
alidai wanapofuatilia kwa lengo la kulipwa fidia, wamekuwa wakizungushwa hivyo
kushindwa kujua hatma yao.
Wakati huo
huo: Waziri huyo amewataka wakuu wa wilaya nchini kushiriki mikutano ya vijiji
na kutoa ardhi kwa wawekezaji ili kuondoa malalamiko ya wananchi.
Alisema
wakuu hao wanatakiwa kuwadhibiti baadhi ya viongozi wa vijiji ambao wamekuwa
wakighushi mikutano hiyo na kuuza ardhi ya vijiji kwa wageni bila kupita kwenye
mkutano mkuu wa kijiji.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment