Meneja Mahusiano wa Kampuni ya simu ya
Airtel, Jackson Mmbando (kushoto), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ushirikiano wa Airtel na
Finca kutoa huduma za kifedha. Kutoka kulia ni , Vivian Temi na Meneja
wa Huduma ya Airtel Money, Stephen Kimea.
Meneja wa Huduma ya Airtel Money, Stephen Kimea (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu huduma hiyo. Kulia ni Msimamizi
Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya Finca Microfinance, Vivian
Temi, Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam, Sarah Daffa na Meneja
Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.
Msimamizi Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya Finca Microfinance, Vivian Temi (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam, Sarah Daffa. |
Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam, Sarah Daffa akizungumza katika mkutano huo.
Maofisa wa Airtel na Finca wakionesha bango wakati wa uzinduzi wa mpango huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya simu za mkononi Airtel Tanzania imesaini makubaliano na benji ya Finca
Microfinance kwaajili ya kuwezesha wateja kuzifikia pesa zao kirahisi kwa
kupitia simu zao za mkononi.
Huduma
hiyo mpya itawawezesha wateja wa Airtel kutuma pesa kutoka kwenye akaunti za
benki kwenda kwenye akaunti zao za Airtel Money na kutoa kwenye simu kwenda
benki.
Akizungumza
Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Meneja Uhusiano wa
Airtel Jackson Mmbando alisema huduma hiyo inalenga kuwawezesha wateza wao
kufanya miamala yao mbalimbali ya kifedha wakati wowote kwa usalam azaidi.
Alisema
kwa kutambua finca sasa ni taasisi ya kibenki wameona ni vyema kuungana na
kuweza kutoa huduma za kuhamisha pesha kwa usalama na kwa ghalama nafuu kupitia
simu za mkononi kwa wateja wao nchi nzima.
"Airtel
itaendelea kuboresha huduma zake ili kuweza kufikia mahitaji ya wateja wake kwa
kushirikiana na mashirika na taasisi mbalimbali katika kuboresha huduma zao kwa
wateja," alisema.
Naye
Meneja wa Kanda wa Finca Microfinance Benki, Sarah Daffa alisema huduma hiyo
itawasaidia katika kuongeza ufanisi kwenye huduma zao.
"Tunawashukulu
Airtel kwa kuungana nasi kupitia huduma za Airtel Money, tunaimani ushirikiano
utatuwezesha kuongeza idadi ya wateja wetu tu bali utasaidia kuongeza idadi ya
miamala inayofanyika kwa urahisi na salama," alisema.
"Wateja
wetu sasa wataweza kufanya miamala ya pesa wakati wowote mahali popote mara
nyingi zaidi ikiwa tu watasajiliwa kweye huduma hiyo na akaunti yake ya benki
ikiwa hai," alisema.
0 comments:
Post a Comment