Mjumbe wa Bodi ya
Filamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bi.Vicensia Shule(wa kwanza
kutoka kushoto) akimwuliza jambo Mwenyekiti wa makampuni ya
Proin Bw,Johnson Lukaza(hayupo pichani) leo jijini Dar es salaam
walipotembelea kujionea miundombinu ya kampuni
hiyo.Kutoka kulia ni Makamu mwenyekiti wa wa Bodi iyo
Bw.Sylvester Sengerema na katikati ni Bw.Bishop Hiluka.
Mtendaji Bodi ya
Filamu Tanzania Bi,Joyce Fissoo akichangia jambo wakati walipotembelea
miundombinu ya Filamu ya Makampuni ya Proin.Bi Fissoo ametoa wito kwa
makampuni yanayotengeneza Filamu Tanzania kuendelea kushirikiana na
Serikali ili kuimarisha Tasnia ya Filamu na kusaidia katika kupambana na
Changamoto mbalimbali.
Mwenyekiti wa Makampuni
ya Proin Bw,Johnson Lukaza akimwonyesha Katibu mtendaji wa Bodi ya Filamu
Bi,Joyce Fissoo moja ya Kazi walizotengeneza na kuingia Sokoni,Pia
aliiomba Serikali kusaidia kuweka sheria kali zitakazo zuia wizi wa Filamu
nchini.
Wajumbe wa Bodi ya
Filamu Tanzania wakifurahia jambo na Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin
Bw,Johnson Lukaza(wa tatu kutoka kushoto) walipotembelea miundombinu ya
kutengenezea filamu ya Kampuni iyo eneo la Mabibo jijini Dar es
Salaam.Wajumbe hao walijionea jinsi Filamu inavyotengenezwa na pia
walitembelea eneo kampuni iyo wanapojenga Studio ya kutengenezea Filamu.
0 comments:
Post a Comment