Shirika la Kuhudumia
Watoto la Umoja wa Mataifa (Unicef) limesema kuwa athari za mgogoro unaoendelea
hivi sasa huko Burundi dhidi ya watoto zinatia wasiwasi mkubwa.
Unicef
limeeleza katika ripoti yake kuwa mgogoro wa Burundi umeifanya hali ya maisha
ya raia wa nchi hiyo hususan watoto kuwa ya mashaka zaidi.
Johannes Wedening
Mwakilishi wa Unicef nchini Burundi amesema kuwa watoto waliokuwa wakishiriki
kwenye maandamano nchini humo wamejeruhiwa vikali na vikosi vya serikali, jambo
ambalo linaashiria namna familia zilivyokandamizwa na vikosi vya usalama vya
Burundi.
Ripoti ya Unicef imeongeza kuwa idadi kadhaa ya shule za Burundi bado
zimefungwa kutokana na machafuko.
Unicef imesisitiza kuwa hali ya mambo ya
Burundi hivi sasa imeboreka kwa kiasi kikubwa na kwamba hatua zimepigwa katika
kuboresha sekta za afya na tiba nchini.
Tangu tareheh 26 Aprili mwaka huu
Burundi imekuwa ikishuhudia maandamano ya wananchi wanaopinga hatua ya Rais
Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo ya kuamua kugombea kiti cha urais kwa duru
nyingine ya tatu. Watu karibu 70 wameuawa na mamia ya wengine kukimbilia katika
nchi jirani kufuatia machafuko hayo.
0 comments:
Post a Comment