Katika
kuonyesha kuwa Benki ya Posta Tanzania (TPB), inafanya inatoa huduma za
kibenki, lakini pia iko mstari wa mbele kuwajali wateja wake na
wananchi kwa ujumla. Katika kutekeleza hilo, wafanyakazi wa benki hiyo,
wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Sabasaba Moshingi, wamejitolea damu,
"kutunisha" benki ya taifa ya damu na hivyo kuokoa maisha ya watanzania
ambapo miongoni mwao ni wateja wake. Zoezi la kutoa damu lilifanyika
makao makuu ya benki hiyo barabara ya Samora jijini Dar es Salaam.
Pichani Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi, akiwaongoza
wafanyakazi wake, katika zoezi hilo.
Mtaalamu
wa masuala ya damu, (kushoto), akimpatia maelezo Meneja Mkuu
anayeshughulikia masuala ya kampuni, Norvis Moes, kuhusu utoaji damu
Moshingi, (kushoto), na mmoja wa wafanyakazi wa TPB, wakitolewa damu kwenye zoezi hilo.
0 comments:
Post a Comment