Ripoti mpya kuhusu maambukizi ya virusi vya UKIMWI

21:08 by Kwetuhouse Media



Ripoti mpya ya Shirika linalohusika na masuala ya Ukimwi katika Umoja wa Mataifa, UNAIDS na Kamisheni ya Lancet, imesema kuwa nchi ambazo zimeathiriwa zaidi na HIV ni lazima zijidhatiti katika kuzuia maambukizi mapya na kupanua upatikanaji wa matibabu ya dawa za ARV.

Ripoti hiyo imesema kuwa bila kufanya jitihada hizo nchi hizo zitakuwa katika hatari ya maambukizi na vifo Ukimwi kutokana na Ukimwi kuliko miaka mitano ilyopita.

Ripoti hiyo iitwayo, 'Kushinda Ukimwi- kuendeleza afya duniani' inaonesha kuwa, ingawa hatua zimepigwa katika kuongeza idadi ya watu wanaotibiwa kote duniani dhidi ya HIV, lakini kiwango cha maambukizi mapya ya HIV hakijashuki haraka ipasavyo.

Aidha, ripoti hiyo imeeleza kwamba maambukizi hayo, pamoja na kuongezeka idadi ya watu katika nchi zilizoathiriwa, kunaongeza idadi ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi, na ambao watahitaji matibabu ya ARV ili waendelee kuishi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Michel Sidibé, amesema kuwa sasa ndio wakati wa kuchukua hatua, na miaka mitano ijayo itatoa fursa ya kuongeza kasi ya jitihada, ili kutokomeza Ukimwi ifikapo mwaka 2030, na la sivyo, athari zake kwa binadamu na kwa uchumi zitakuwa ni janga.

0 comments:

Post a Comment