Zitto,salaam.Hongera
pia kwa kuwa kiongozi wa ACT na hongera kwa kazi kubwa unayoifanya kueneza
itikadi ya Chama chako.Ni jambo zuri katika kukuza demokrasia ya nvhi yetu na
hasa kukuza uzalendo.Siku zote nimekuelezea kama kijana ambaye hakika utakuwa
tegemeo la Taifa letu,na hili nimekuambia mara nyingi.
Nimeona
vema nifafaanue yale ambayo umeyataja katika post yako. Niliystolea maelezo ya
kina miaka mingi iliyopita lakini nadhani utafiti sio moja ya maeneo tuliyo na nguvu
nayo kwa hiyo umeyafukua bila kuyafanyia utafiti au kutaka upate ufafanuzi
kutoka kwa mhusika.
Nianze na
hili la ubinafsishaji kwa ujumla wake.Inawezekana ulikuwa badi shule,pamoja na
nia njema ya kuanzisha mashirika ya umma,hatimaye yalikuja kuwa mzigo mkubwa
kwa hazina yetu,maana yake kwa wanachi.
Asilimia
kubwa yalitegemea ruzuku ya serikali na baadhi yalikuwa mufilisi. Teknolojia
ilikuwa imebadilika sana na ili kuyafugua ingeigharimu serikali na umma wa
Tanzania kiasi kikubwa sana.
Uchumi wa
nchi wakati ule usingeweza kubeba mzigo huo.Ndipo Chama,wakati ule kiliporidhia
Serikali ibakie na shughuli zake za msingi za Utawala,Ulinzi na Usalama,na
Usimamizi wa ujumla wa uchumi.
Maamuzi
yafuatayo yakachukuliwa: Kwa upande wa shughuli za serikali zenye sura ya
kibiashara, idara husika zikageuzwa kuwa wakala wa serikali, zikifanya kazi kwa
uhuru zaidi chini ya Bodi zao. Kuhusu mashirika na kampuni za umma ilikubalika
zirekebishwe na hatimaye zibinafsishwe.
Ndipo
kilipoundwa chombo maalum kisheria kilivhokuwa na mamlaka kamili ya
kubinafsisha mashirika, kwa mashirika yaliokuwa yanahusu wizara yako, hii bodi
ya ubinafsishaji ilikushirikisha ama la? Kwasababu kama shirika la ndege na
TTCL vimekufa kabisa baada ya kubinafsishwa.
Mashirika
ya umma.Chombo hiki Parastatal Sector Reform Commission,PSRC, kilikuwa chombo
huru kikiwa chini ya Ofisi ya Rais,Mipango. Kiliwekwa hapo kwa sababu mamlaka
yake yalikuwa Mtambuka,na vyombo husika vilikuwa kwenye sekta mbalimbali.
Kwa hiyo
sekta husika na Wizara husika,pamoja na kuitwa PSRC waksti wa majadiliano
yaliyohusu mashirika yake,hazikuwa na mamlaka ya kisheria kuhusu ubinafsishaji.
Ni vema
hili likaeleweka.Pamoja na hayo,nirudie ufafanuzi kuhusu ubinafsishaji wa
TTCL,nafanya hivyo kutokana na dhana ya uwajibikaji wa pamoja, ikumbukwe kwamba
maamuzi ya ubinafsishaji wa TTCL yalifikiwa na PSRC mwaka mmoja kabla Waziri
Mwandosya hajaingia siasa!Hata hivyo suala kubwa ni mabadiliko ya teknolojia
yetu.
TTCL
ilikuwa imejikita zaidi kimfumo na kiteknolojia katika teknolojia ya analogue
na land lines.Mfumo wate,kiutawala na kiteknolojia ulikuwa katika msingi
huo.Teknolojia ya simu za mkononi,na ushindani uliojitokeza ndio hasa
changamoto kubwa ya TTCL.
Hsta hivyo
mabadiliko makubwa na maendeleo makubwa katika TEHAMA yamepelekea Tanzania kuwa
mbali na kuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingi za Afrika.
Katika
mawasiliano Tanzania imekuwa 'Mecca' na wengi wamekuja kujifunza tumewezaje
kufanikiwa.Namshukuru Rabuka kwa kuniwezesha kutoa mchango wangu katika
maendeleo ya sekta hii. Na ili kuhakikisha kwamba mlaji au mtumiaji wa huduma
za kiuchumi hahujumiwa na wakati huo huo mtoa huduma au mwekezaji anauhakika wa
kufaidika na kuweza kutoa huduma endelevu,ndipo vilipoanzishwa vyombo vya
udhibiti wa huduma za kiuchumi,Regulatory Bodies.
Nimebahatika
kuwa Waziri pekee mwanzilishi na msimamizi wa TCRA, SUMATRA, TCAA, na EWURA.
Nimeelezea kuhusu mfumo wa ubinafsishaji hivyo basi ninachoweza kufafanua ni
kwamba nilipomaliza muda wangu kama Waziri wa Mawasiliano na Uchukuxi, niliacha
Shirika la Reli likisafirisha tani laki tisa za shehena kwa mwaka,safari za
abiria kwenda Tabora kutoka Dar zilikuwa kila siku,na ATC ilikuwa na ndege
mbili aina ya Boeing 737 na mbili aina ya Fokker Friendship.Tuhuma za mtoto wa
Prosesa kulipiwa na kampuni moja ya simu hazina chembe yoyote ya ukweli Bwana
Zitto. Mtoto ambaye alifuzu uhandisi wa mawadiliano ya simu aliomba kazi ya
muda na akapewa.
Kampuni husika ilikanusha tuhuma hizo ambazo zilitolewa
wakati wa mchakato wa kugombea uteuzi katika CCM kwa nafasi ya kuwa mgombea wa
Urais mwaka 2005.S,asa zinafufuliwa tena na Bwana Zitto wakati wa mchakato huo
huo mwaka 2015! Inaeleweka.
Namalizia kama nilivyoanza,Zitto ni mwanasiasa
ninayemheshimu sana.Mara nyingi naye amenitambua kama mwanasiasa wa kuigwa(role
model).Lakini katika siasa tunasema saa 24 ni kipindi kirefu sana,na huwa
tunabadilika!Ushauri wangu kwake ni kwamba siku zote kabla hujahukumu sikiliza
upande wa pili,kwa kilatini hii ni dhana muhimu inayojulikana kama AUDI ALTERAM
PARTEM.Pili ni vema ukazingatia zaidi mambo chanya ya msimamo na itikadi ya
ACT.Lakini katika kushauri hivyo natambu kwamba " akili ni nywele,kila mtu
ana zake" Ramadhan Kareem.Wakatabahu, Mwandosya
0 comments:
Post a Comment