Muonekano
wa nje wa Banda la Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), Tanzania lililopo
ndani ya Karume Hall wanaoshiriki katika Maonesho ya 39 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam ya sabasaba yaliyoanza kurindima jana kwenye
katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini
Dar.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Afisa
habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma
Ledama akitoa maelezo ya taarifa mbalimbali zilizoorodheshwa kwenye
jarida la vijana lililoandaliwa na Shirika linaloshughulikia idadi ya
watu Duniani (UNFPA) kwa mmoja wa wakinamama aliyetembelea banda kwa
ajili ya kufahamu shughuli mbalimbali na mchango wa shirika la Umoja wa
Mataifa kwa serikali Tanzania.
Modewji blog team, Sabasaba
Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), Tanzania wapo katika maonyesho ya 39
ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyoanza kurindima mapema
jana.
UN
Tanzania ambao wapo katika banda la Karume ndani ya mabanda hayo ya
Sabasaba, kutoa elimu inayolenga kuionyesha jamii mafanikio, changamoto
na fursa zilizopo katika Umoja wa Mataifa ambapo mwaka huu unafikisha
miaka 70 tangu shirika hilo lianzishwe.
“Huu ni mwaka muhimu sana kwani safari ya Umoja wa Mataifa ilianza
mwaka 1945, hadi kufikia sasa kuwa umefikia wapi, tupo wapi na
tunaelekea wapi katika kushughulikia changamoto za kidunia ikiwemo
Amani na usalama, changamoto za maendeleo, changamoto za mabadiliko ya
tabia nchi, na changamoto zingine”, alieleza Afisa Habari wa kituo cha
Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama.
Aidha,
alibainisha kuwa, UN ambayo imeweza kufikisha miaka 15 ya malengo ya
Milenia yaliyokubaliwa na nchi wanachama wa Umoja huo mwaka 2000,
yanafikia kilele hapo Desemba 30, mwaka huu hivyo wakuu hao wanchi
watakutana tena mwezi Septemba mwaka huu, kupanga malengo mapya ya
Maendeleo endelevu (SDGs) ambayo yatakapokubalika yataanza kutumika
mwakani.
“Huu ni mwaka muhimu sana. wa kuonyesha hayo mabadiliko, tumekuwa na
miaka 15 ya milenia kuna vitu tumefanikiwa na tumekuwa na changamoto.
Kwa hiyo malengo hayo yalikuwa ni shirikishi kutoka kwa kada
zote”alieleza.
Pia
alieleza kuwa katika mkutano mkubwa wa mabadiliko ya tabianchi ambao
utakuwa mkutano mkubwa wa 21, utakaofanyika Paris-Ufaransa Disemba
mwaka huu. Wakuu wa nchi watakuja na makubaliano ya kuona watafanya nini
hivyo makubaliano hayo ni muhimu sana.
Nchi zote duniani zimeona suala la mabadiliko ya tabianchi si la
nadharia tena bali ni la wote kuungana kupambana nalo kwani wote
tunaathirika.
Hivyo
tunawakaribisha sana watanzania kutembelea katika banda letu kujionea
na kufahamu na kujifunza na kwa Tanzania mwaka huu tunamalizia program
yetu ya kwanza ambayo tunashirikiana mashirika yote kufanya kazi kwa
pamoja (Delivering as one) katika kutatua changamoto zinazotukabili hapa
Tanzania kwa kushirikiana na serikali.
Afisa
habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma
Ledama akisikiliza swali kutoka kwa raia wa kigeni mwenye asili ya asia
aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya sabasaba
yaliyoanza kurindima jana katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Afisa
habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma
Ledama akiendelea kuwapiga msasa raia hao wa kigeni waliotembelea banda
la shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania.
Afisa
habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma
Ledama akisaidiana na mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la Umoja wa
Mataifa kwenye maonyesho ya sabasaba kukusanya machapisho na vipeperushi
mbalimbali vinavyoelezea shughuli za Umoja wa Mataifa.
Baadhi
ya wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania katika hatua
za mwisho za kuandaa program mbalimbali zitakazokuwa zikitoa elimu kwa
wananchi wakataotembelea banda hilo katika maonyesho ya sabasaba
yaliyoanza kutimua vumbi jana katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Pichani
juu na chini ni meza zilizosheheni ripoti, vitabu na majarida
mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kwa ajli ya watanzania kujisomea na
kuelimika kuhusiana na shughuli na taarifa mbalimbali za ustawi wa
kidunia zinazofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa.
0 comments:
Post a Comment