Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP), John Minja akimkarisha Rais
Jakaya Kikwete (kushoto) katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza,
Ukonga jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufunga mafunzo ya uofisa wa
Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Jeshi hilo. Maafisa 104 wa kozi hiyo
walihitimu mafunzo hayo na kuvishwa vyeo hivyo. Kulia ni Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia),
akimkarisha Rais Jakaya Kikwete kuketi baada ya kukagua gwaride la
wahitimu 104 wa kozi ya Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Magereza kabla ya
Rais huyo kuyafunga mafunzo hayo katika sherehe iliyofanyika katika
Viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP), John Minja, na kulia
ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick.
Rais Jakaya Kikwete akimvisha muhitimu Amina Lidenge, Cheo cha
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Magereza kwa niaba ya wenzake 104
waliomaliza mafunzo hayo katika Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga
jijini Dar es Salaam. Rais Kikwete aliyafunga mafunzo hayo ambayo
yalienda sambamba na Siku ya Magereza ambapo baada ya kuyafunga aliweza
kutembelea mabanda na kuonyeshwa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na
jeshi hilo nchini.
Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride liloandaliwa kwa ajili yake na
wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza
kabla ya kuyafunga mafunzo ya Cheo cha Mrakibu Msaidizi yaliyofanyika
katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es
Salaam. Rais Kikwete aliyafunga mafunzo hayo ambayo yalienda sambamba na
Siku ya Magereza ambapo alikagua bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na
jeshi hilo nchini.
Kikosi cha Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu
wa Jeshi la Magereza kikipita mbele ya Jukwaa Kuu kutoa heshima kwa
mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) katika sherehe ya
ufungaji wa mafunzo hayo ya Cheo cha Mrakibu Msaidizi yaliyofanyika
katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es
Salaam. Wahitimu 104 walivishwa cheo hicho. Ufungaji wa mafunzo hayo
yalienda sambamba na Siku ya Magereza ambapo Rais KIkwete alikagua
bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na jeshi hilo nchini.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP), John Minja akitoa hotuba yake
kabla ya Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kuyafunga mafunzo ya
Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo pamoja na kuwavisha vyeo vya
Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo. Katika hotuba yake CGP
Minja alisema jeshi lake linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo
ukosefu mkubwa wa nyumba za askari na maafisa Magereza.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akitoa hotuba fupi
pamoja na kumkaribisha Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kwa ajili ya
kuzungumza na askari, maafisa wa Jeshi la Magereza pamoja na wageni
waalikwa na baadaye kuyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa
Jeshi hilo pamoja na kuwavisha vyeo cha Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa
jeshi hilo. Katika hotuba yake Waziri Chikawe alisema Jeshi hilo
linakabiliwa na upungufu mkubwa wa magereza.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Askari na Maafisa wa
Jeshi la Magereza, wageni waalikwa na wananchi wakati akiyafunga mafunzo ya
Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo na kuwatunukia vyeo vya Warakibu
Wasaidizi 104. Katika hotuba yake Rais Kikwete aliwapongeza wahitimu hao kwa
kutunukiwa vyeo hivyo, na pia aliwataka maafisa wa Jeshi hilo wafuate sheria
kwa wawatendea haki Mahabusu na Wafungwa katika magereza nchini
Kikosi Maalumu cha Ukakamavu cha Jeshi la Magereza (KMKM)
kikimuonesha Rais Jakaya Kikwete na wageni waalikwa (hawapo pichani) jinsi
kikosi hicho kinapokuwa kazini wakati wanapopambana na wahalifu wa aina
tofauti. Rais Kikwete aliyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi
hilo pamoja na kuwavisha vyeo vya Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo
katika sherehe iliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza,
Ukonga jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha gwaride wa Askari wa Jeshi la Magereza la zamani
(askari jela) likionyesha jinsi kipindi cha zamani jeshi hilo lilivyokuwa
linafanya gwaride lake katika sherehe na shughuli mbalimbali za Jeshi hilo.
Tukio hilo lilifanyika kabla ya Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kuyafunga
mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo pamoja na kuwavisha vyeo vya
Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo katika sherehe iliyofanyika katika
Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete (wakumi kushoto-waliokaa) akiwa katika
picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Maafisa wa Jeshi la Magereza, wahitimu pamoja na wageni waalikwa, baada ya
kuyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo pamoja na kuwavisha
cheo cha Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi hilo.
Rais Jakaya Kikwete akiiangalia bilinganya wakati alipokuwa anatembelea
mabanda yenye bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Jeshi la Magereza nchini. Rais
Kikwete alitembelea maonyesho hayo maalumu yanayofanyika kila mwaka katika Siku
ya Magereza, mara baada ya kuyafunga mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa
Jeshi hilo pamoja na kuwavisha vyeo vya Mrakibu Msaidizi wahitimu 104 wa jeshi
hilo, katika tukio lililofanyika Uwanja wa Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo,
Ukonga jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Kilimo wa Jeshi hilo, Yesaya
Kitundu. Wapili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe,
na anayefuata ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick. Picha zote na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 comments:
Post a Comment