Mkurugenzi
Mtendaji mpya wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Tausi Kida, akitoa maelezo ya kongamano kabla ya kumkaribisha mgeni
rasmi kulifungua kongamano kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa
linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs)
limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma ambalo liliandaliwa na
taasisi yake.
Kamishna
wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha, Ngosha Magonya akisoma hotuba ya
ufunguzi wa kongamano hilo kwa niaba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu wa
wizara hiyo katika hoteli ya St. Gasper mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
KONGAMANO
kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza
malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika mwishoni mwa wiki
mjini Dodoma.
Kongamano
hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya Masuala ya Uchumi na jamii
(ESRF) limelenga kuwakutanisha wataalamu kutoka Tanzania Bara na
Visiwani kujadili namna ya kupata fedha za kutekeleza malengo hayo baada
ya kumalizika kwa malengo ya maendeleo ya millennia (MDG’s) baadae
mwaka huu.
Miongoni
mwa mambo yaliyojadiliwa katika kongamano hilo ambapo wataalamu wa
Umoja wa Mataifa wa maendeleo walishiriki ni pamoja na namna ya kupata
fedha kwa ajili ya maendeleo baada ya Septemba mwaka 2015 kwa kuangalia
rasilimali za ndani.
Mada
hiyo imetokana na ukweli kuwa upatikanaji wa fedha za ndani ndio suluhu
ya utekelezaji wa malengo mapya kwa kuwa awali kwenye MDG’s utekelezaji
wa malengo ulikwamishwa na kukosekana kwa fedha kutoka kwa wafadhili
ambao waliahidi kuchangia maendeleo.
Pamoja
na kuangalia upatikanaji wa fedha kutekeleza malengo hayo mapya bila
kuacha yale ya zamani, washiriki pia waliangalia namna ya kujiandaa
katika ufuatiliaji wa malengo ya Maendeleo endelevu (SDG’s).
Mkurugenzi
Mtendaji mpya wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Tausi Kida, akitoa maelezo ya kongamano kabla ya kumkaribisha mgeni
rasmi kulifungua katika ukumbi wa mikutano hoteli ya St Gasper mjini
Dodoma alisema kuwapo kwa kongamano hilo kumetokana na haja ya
kujiandaa kabla ya mkutano wa tatu wa namna ya kutafuta fedha kwa ajili
ya miradi ya maendeleo.
Mkutano huo utafanyika mwezi ujao mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Aidha alisema kwamba upo umuhimu wa kuangalia uimarishaji wa ushirikiano wa dunia katika kuimarisha maendeleo endelevu.
Dk.
Kida alisema kwamba kongamano hilo ambalo ni sehemu ya maandalizi ya
kuingia katika SDGs; na kuwa taasisi ya ESRF kwa miaka mitatu imekuwa
likifuatilia katika kuratibu mazungumzo kuhusu hatima yam MDG’s baada ya
2015.
Akifungua
mkutano huo Katibu mkuu Hazina Dk. Servacius Likwelile aliwataka
washiriki kuhakikisha kwamba wanachambua masuala muhimu yanayohusu
maendeleo na kuyawekea mkakati katika mkutano ujao wa Addis Ababa,
Ethiopia.
Akisoma
hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu, Kamishina wa Fedha kutoka Nje Wizara
ya Fedha Ngosha Magonya amesema kwamba amefurahishwa na juhudi za ESRF
kuwakutanisha wataalamu kujipanga kwa mikutano ijayo na utekelezaji wa
maendeleo endelevu ya SDG’s.
Aidha
aliipongeza taasisi ya United Nations Development Programme (UNDP) kwa
kusaidia Tanzania kuangalia hali ilivyokuwa katika MDG’s na hali ya
baadae.
Mtaalamu
wa masuala ya uchumi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
Dar es salaam, Rogers Dhliwayo akitoa salamu za Shirika la Umoja wa
Mataifa la Maendeleo (UNDP) wakati wa kongamano hilo la siku mbili la
kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya
Maendeleo endelevu (SDGs) lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Afisa
Mwandamizi wa uhamasishaji na uwekezaji kutoka kituo cha uwekezaji
nchini (TIC), Lilian Mwamdanga akishiriki kuchangia maoni wakati
kongamano kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa
kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika
mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Naibu
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)-
Programme, Amon Manyama akichangia maoni wakati wa kongamano kubwa la
siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo
mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika mwishoni mwa wiki mjini
Dodoma.
Mkurugenzi
Mtendaji mpya wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Tausi Kida na Kamishna Mipango wa Tume ya Mipango Zanzibar, Ahmed
Makame Haji wakifuatilia kwa umakini maoni mbalimbali ya wadau
yaliyokuwa yakitolewa kwenye kongamano hilo.
Pichani
juu na chini ni washiriki kutoka Tanzania bara na visiwani walioshiriki
kongamano hilo la siku mbili ambalo liliandaliwa na taasisi ya ESRF.
Naibu
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)-
Programme, Amon Manyama (kushoto) akizungumza jambo na Kamishna wa Fedha
za Nje wa Wizara ya Fedha, Ngosha Magonya ambaye amemwakilisha mgeni
rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha (wa pili kushoto) wakati akiondoka
katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Saint Gasper mjini Dodoma mara
baada ya kufungua kongamano kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa
linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDG's)
lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma. Wengine katika picha
kutoka kulia ni Kamishna Mipango wa Tume ya Mipango Zanzibar, Ahmed
Makame Haji, Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi Huru ya Utafiti wa
Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida pamoja na Mtaalamu wa masuala ya
uchumi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam,
Rogers Dhliwayo.
Mkurugenzi
Mtendaji mpya wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Tausi Kida (kushoto) akimsindikiza Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara
ya Fedha, Ngosha Magonya ambaye alimwakilisha mgeni rasmi Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha mara baada ya kufungua kongamano kubwa la siku mbili la
kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya
Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Picha ya pamoja ya washiriki.
0 comments:
Post a Comment