HOTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR NA
MWENYEKITI WA BARAZA LA
MAPINDUZI
MHESHIMIWA DK. ALI MOHAMED SHEIN,
WAKATI WA KULIVUNJA BARAZA LA
NANE LA
WAWAKILISHI, TAREHE 26 JUNI, 2015
Mheshimiwa Pandu
Ameir Kificho,
Spika wa Baraza
la Wawakilishi,
Mheshimiwa
Balozi Seif Ali Iddi,
Makamu
wa Pili wa Rais,
Mheshimiwa
Omar Othman Makungu,
Jaji
Mkuu wa Zanzibar,
Waheshimiwa
Wenyeviti wa Baraza la Wawakilishi,
Waheshimiwa
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi,
Waheshimiwa
Mabalozi wadogo mlioko Zanzibar,
Wawakilishi wa
Mashirika mbali mbali ya Kimataifa,
Waheshimiwa
Viongozi wa Vyama vya Siasa,
Ndugu Wageni
Waalikwa,
Mabibi na
Mabwana,
Assalam Aleikum
UTANGULIZI:
Mheshimiwa
Spika,
Awali
ya yote, naanza hotuba yangu kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu; Mwingi wa Rehema na
Utukufu kwa kutujaalia afya njema na uhai tukaweza kukutana katika hadhara hii
muhimu. Namuomba Mwenyezi Mungu atujaalie kila la kheri katika utekelezaji wa
wajibu wetu huu wa kikatiba.
Kadhalika,
nawapa pole wale wote walioathirika na maafa ya kipindi cha mvua kubwa za hivi
karibuni zilizopelekea watu watatu kupoteza maisha na wengine kupoteza mali na
uharibifu mkubwa wa nyumba na mazingira. Aidha, tunawashukuru wale wote
walioungana na Serikali katika kutoa misaada mbali mbali ya kuwafariji ndugu
zetu waliofikwa na maafa hayo. Tunawaomba ndugu zetu hao walioathirika
waendelee kuwa na nyoyo za subira na Mwenyezi Mungu awape uwezo wa kukabiliana
na mitihani iliyowasibu.
Mheshimiwa
Spika,
Napenda
kutoa shukrani za dhati kwako na Baraza lako tukufu kwa kunipa nafasi hii ya
kuja kulihutubia Baraza hili la Nane kabla ya kulivunja. Kwa hivyo, kikao hiki
cha leo kimeitishwa kwa ajili ya kutekeleza matakwa ya Kikatiba kwa mujibu wa
mamlaka niliyopewa katika Kifungu cha 91(2) (a) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka
1984. Kadhalika, kikao chetu hiki ni utekelezaji wa Kifungu cha 92(1) cha
Katiba ya Zanzibar kuhusiana na uhai wa Baraza la Wawakilishi kuwa ni kipindi
cha miaka mitano tangu ulipoitishwa mkutano wa kwanza na leo tarehe 26 Juni,
2015 ndiyo nalihutubia Baraza la Nane kwa mara ya mwisho kabla ya kulivunja ili
kupisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Napenda
nitumie fursa hii ili nitoe shukrani zangu za dhati kwako Mheshimiwa Spika kwa
uongozi wako bora na kwa kazi kubwa uliyoifanya katika kipindi cha miaka mitano
ya Baraza hili, kwa kusimamia na kwa kuziendesha kazi za Baraza kwa mafanikio
makubwa. Hongera sana.
Shukrani
zangu za dhati ziwaendee Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza hili kwa kuzitekeleza
kazi zao kwa moyo wa kujituma, kwa kushirikiana na kwa uvumilivu mkubwa. Ni
imani yangu kwamba wananchi wameridhika na namna mnavyowawakilisha mawazo na
maelekezo yao katika Baraza hili. Licha ya kuwa na wajumbe wapya wengi katika
Baraza hili na upya wa mfumo wa kisiasa tulionao na muundo mpya wa Serikali,
mmeweza kuifanya kazi yenu kwa ufanisi mkubwa.
Mheshimiwa
Spika,
Nachukua
fursa hii, mimi mwenyewe na kwa niaba ya Serikali kutoa mkono wa pole na rambi
rambi kwako, wajumbe wa Baraza lako, ndugu, jamaa na wananchi wa Jimbo la
Magomeni na Watanzania wote kwa kifo cha kiongozi mwenzetu Marehemu Salmin
Awadh Salmin; aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni na Mnadhimu wa CCM hapa
Barazani. Hekima, busara na mchango wake katika kuwatumikia wananchi wa
Zanzibar na kuliendeleza Taifa letu, hautasahaulika na utaendelea kuthaminiwa.
Namuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi - Amin.
Mheshimiwa
Spika,
Katika
hotuba yangu ya uzinduzi wa Baraza hili la Nane tarehe 11 Novemba, 2010,
nilieleza mwelekeo wa mipango ya Serikali nitakayoiunda baada ya wananchi wa
Zanzibar kunichagua kwa kura nyingi, kupitia Chama changu cha Mapinduzi, kuwa
Rais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 31 Oktoba, 2010.
Kadhalika,
katika hotuba yangu hiyo, nilisema kuwa tunaianza Awamu ya Saba ya Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar tukiwa na dhima ya msingi ya kuwatumikia wananchi
waliotuchagua kwa kipindi cha miaka mitano. Matumaini ya wananchi kwa Serikali
yao yalikuwa ni kuyaendeleza mafanikio yote yaliyoletwa na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa awamu zote zilizotangulia na kutekeleza sera na
mipango itakayowezesha kukuza uchumi na kuimarisha ustawi wa jamii.
Ili
kuyafikia malengo hayo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba
inaongozwa kwa kuzingatia mipango mikuu ya kitaifa ambayo ni Dira ya Maendeleo
ya 2020, Malengo ya Milenia, MKUZA na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010
hadi 2015. Sambamba na hayo, utekelezaji wa ahadi nilizozitoa katika kampeni ya
uchaguzi ya mwaka 2010 ilikuwa ni miongoni mwa vipaumbele muhimu katika
utendaji wa serikali niliyoiunda.
Mheshimiwa
Spika,
Leo
nitaelezea kwa muhtasari mafanikio ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu
ya Saba, katika nyanja zote za maendeleo, kisiasa, kiuchumi na ustawi wa jamii.
Ni
dhahiri
kuwa mafanikio hayo yanatokana na mchango wenu katika kutekeleza wajibu,
kufuatana na Mipango mikuu ya kitaifa niliyoeleza hapo mwanzo na Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 – 2015. Ilani hiyo ni mkataba baina ya wananchi
na Serikali yetu. Ni jambo la kufurahisha kwamba hadi leo hii, Ilani hiyo
imeshatekelezwa kwa kiwango kinachokadiriwa kufikia asilimia 90. Natoa pongezi
kwa wale wote walioshiriki katika utekelezaji wa Ilani hii.
Siri
kubwa ya mafanikio yetu ni kuwa sisi tuliingia katika muundo wa Serikali ya
Umoja wa Kitaifa tukiwa tayari tunayo Katiba iliyoandaliwa kwa ajili ya Muundo
huo. Lakini zaidi ya hayo, tulidhamiria kwa dhati kuitekeleza azma na shabaha
ya muundo huo. Tulijenga heshima na mapenzi baina yetu. Tulijenga misingi ya
kuvumiliana. Kwa kufanikisha uendeshaji wa serikali, nilipanga Wizara na kuteua
Mawaziri kwa uwiano wa matakwa ya Katiba ya Zanzibar.
MAFANIKIO YA
UTEKELEZAJI WA MIPANGO YA SERIKALI:
HALI YA UCHUMI:
Mheshimiwa
Spika,
Katika
kipindi hiki kuanzia mwaka 2010 – 2014, Pato la Taifa kwa bei za miaka hio
limekua kutoka TZS bilioni 1,050.8 hadi kufikia TZS bilioni 2,133.5. Kwa bei za
kudumu, Pato la Taifa limekua kutoka TZS bilioni 848.2 hadi kufikia TZS bilioni
1,115.4 sawa na ukuaji wa asilimia 31.5 kwa kipindi hicho. Uchumi wetu umekua
kutoka asilimia 4.3 mwaka 2010 hadi kufikia asilimia 7.0 mwaka 2014 sawa na
ongezeko la asilimia 2.7. Pato la Taifa kwa mwananchi mmoja, kwa bei za miaka
2010 – 2014, limekua kutoka TZS 856,000 ($613) mwaka 2010 hadi kufikia TZS
1,552,000 ($939) kwa mwaka 2014.
Katika
kipindi cha mwaka 2010/2011 hadi 2014/2015, mapato ya ndani yameongezeka kutoka
TZS bilioni 181.4 hadi kufikia TZS bilioni 360.4, sawa na ukuaji wa asilimia
98.7 kwa kipindi hicho au wastani wa asilimia 19.7 kwa kila mwaka.
Mheshimiwa
Spika,
Kwa
upande wa mfumko wa bei, tunaendelea kuwa na mfumko wa bei ulio katika tarakimu
moja. Katika mwaka 2010, mfumko wa bei ulikuwa wa wastani wa asilimia 6.1 na
umeshuka kufikia wastani wa asilimia 5.6 kwa mwaka 2014.
Mheshimiwa
Spika,
Kwa
mwaka wa fedha wa 2015/2016, Bajeti yetu itaendelea kuzingatia malengo makuu ya
Serikali. Malengo hayo ni kujenga jamii: (i) Iliyoelimika kwa elimu bora na
inayotoa wataalamu wenye hadhi ya kimataifa; (ii) Yenye siha, (ii)
Iliyoimarika kiuchumi; na (iv) Inayojali Umoja wa Kitaifa na kufuata misingi ya
Utawala Bora. Mambo haya ndio yanayojenga falsafa iliyomo katika
Dira ya Maendeleo ya 2020 ambayo inatekelezwa kwa sasa kupitia MKUZA II na
Mpango wake wa utekelezaji. Utendaji wa sekta zote umejielekeza katika kufikiwa
kwa malengo hayo makuu.
Mheshimiwa
Spika,
Katika
kuinua uchumi wetu, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha Idara ya
Mipango, Sera na Utafiti katika kila wizara kwa lengo la kutilia mkazo umuhimu
wa utafiti katika maendeleo yetu. Serikali, kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi
na Teknolojia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (COSTECH) imeendeleza tafiti
katika taasisi mbali mbali ikiwemo Kilimo, Elimu, Uvuvi na Nyanja nyenginezo.
MATOKEO KWA
USTAWI: (RESULTS FOR PROSPERITY - R4P)
Mheshimiwa
Spika,
Katika
kutafuta mbinu bora za kutekeleza mipango yetu, Serikali imeanzisha utaratibu
wa kuwakutanisha wataalamu wa sekta mbali mbali kwa mfumo uliopewa jina la
Mpango wa Maabara kwa ajili ya kujadili, kupanga na kupitisha maazimio ya
utelekezaji wa mipango mbali mbali ya maendeleo. Utaratibu huu, hapa petu,
tumeufuata na tumeupa jina la Matokeo kwa Ustawi (Results for Prosperity - R4P)
ambao umeonesha kuwa na mafanikio makubwa kwa nchi zilizouanzisha na kuufuata.
Hivi karibuni Serikali imeanza kutekeleza programu mbali mbali zinazotayarishwa
katika Mpango wa Matokeo kwa Ustawi. Programu zilizoanza kutekelezwa ni pamoja
na Programu Mjumuisho ya
Kuendeleza
Utalii, Programu ya Kuimarisha Mazingira ya Biashara na Mkakati wa Utafutaji
Rasilimali Fedha. Kwa sasa mchakato unaendelea wa matayarisho kwa ajili ya
sekta afya na elimu ambazo tunatarajia zitaanza katika mwaka huu.
MIRADI YA
MASHIRIKIANO BAINA SEKTA YA UMMA NA SEKTA BINAFSI:
Mheshimiwa
Spika,
Katika
kipindi cha miaka mitano, tumefanya jitihada kubwa za kuiimarisha na
kuishirikisha Sekta binafsi katika mipango yetu ya maendeleo. Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar tayari imeanzisha kitengo cha “PPP” katika Tume ya
Mipango kwa ajili ya kushughulikia miradi itakayoanzishwa kwa mfumo huo.
Serikali imejiandaa kuanzisha Idara kamili ya “PPP” ambayo itahusika na
utekelezaji na usimamizi wa shughuli zote za miradi ya mashirikiano baina ya
Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.
UWEKEZAJI VITEGA
UCHUMI:
Mheshimiwa
Spika,
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba, kupitia Mamlaka ya Vitega Uchumi
(ZIPA) ilifanya kazi nzuri katika kuwavutia wawekezaji wa nje na ndani kuja
kuwekeza katika sekta mbali mbali za kiuchumi na kijamii. Kwa Kipindi cha miaka
mitano (2010 – 2015), tumeweza kusajili miradi 187 yenye thamani ya TZS milioni
38,560.50, sawa na USD 1,881,00 milioni ambayo inakadiriwa kuwapatia ajira watu
9,192. Wawekezaji kutoka Uturuki, China, Italia, Ujerumani na India wameonesha
dhamira ya dhati ya kutuunga mkono na nimetumia fursa niliyoipata kuwakaribisha
waje kuwekeza, wakati nilipotembelea nchi zao, vile vile wawekezaji wa ndani
nao wamehamasika katika uwekezaji kwenye nyanja mbali mbali.
Mheshimiwa
Spika,
Serikali
kupitia Mamlaka ya Uwekezaji na Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA), kuanzia mwaka wa
fedha 2014/2015, imeweka mkazo mkubwa katika kukamilisha dhamira ya kuendeleza
maeneo huru ya uchumi. Ni dhahiri kwamba mpango huu tangu ulipobuniwa na
hatimae kutolewa tangazo la Sheria Namba 5 la mwaka 1993 bado
hazijachukuliwa
juhudi za kutosha za kutekeleza kwa vitendo uendelezaji wa maeneo hayo.
Kwa
hakika hivi sasa tumejidhatiti kuitekeleza dhana ya maeneo huru ya uchumi kwa
vitendo. Mipango yetu ni kuibadilisha taswira ya eneo la Fumba. Tumepanga
kuutekeleza Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Kisasa wa Fumba (Fumba Bay Satellite City
Project). Mji huu mpya wa kisasa na wa kibiashara utakuwa na mtaa mkubwa wa
biashara (High Street), nyumba za kisasa za kibiashara za kuishi wageni na
wenyeji na uwanja wa kuchezea mchezo wa gofu. Vile vile, kutakuwa na hoteli
moja kubwa ya nyota tano yenye vyumba 400 na tutajenga eneo la shughuli za
biashara ambalo litakuwa na maghala ya kisasa na mfumo wa usafirishaji wa
bidhaa wa kisasa.
Aidha,
katika mji huu kutakuwa na uwanja wa mpira wa kisasa ambao utakuwa na uwezo wa
kuchukua kiasi cha watu 45,000. Pamoja na huduma za kijamii za ulinzi, afya na
elimu, mradi huo unakusudia kuanzisha bandari ndogo kwa ajili ya huduma za
usafiri wa majini kati ya Zanzibar - Pemba na Zanzibar - Dar es Salaam. Jumla
ya hekta 700 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu. Serikali imeanza
mazungumzo na Muwekezaji wa Kampuni mama ya Bakhresa Group juu ya kushirikiana
katika uwekezaji wa mradi huu kwa mfumo wa ubia (joint venture company).
Mheshimiwa
Spika,
Vile
vile, katika eneo hili tutatekeleza Mradi wa Mtaa wa Viwanda. Jumla ya hekta
100 zimetengwa katika maeneo ya Dimani, Kusini pamoja na Ndambani kwa ajili ya
uendelezaji wa shughuli za viwanda vidogo na vya kati. Mazungumzo yanaendelea
kati ya Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) na Kampuni ya CPC ya Misri juu
ya mfumo na utaratibu na ushirikiano wa uwekezaji wa Miundombinu katika eneo
hilo.
Kadhalika,
Hekta 60 zimetengwa kwa ajili ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano na
kukabidhiwa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko kwa ajili ya kuandaa maelezo
maalum ya mradi wa uwekezaji. Maelezo hayo yakiwa tayari, Mamlaka itashirikiana
na Wizara hiyo kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi katika uwekezaji
utakaopangwa.
Mheshimiwa
Spika,
Vile
vile, Serikali imebuni mpango wa kutekeleza Mradi wa Uendelezaji wa Mji wa
Nyamanzi – Fumba. Mradi huu umetengewa kiasi cha hekta 63 ambazo zitatumika kwa
ajili ya nyumba za makaazi na biashara mbali mbali ikiwemo maeneo ya makaazi ya
kijamii, majengo ya kuishi, huduma za hoteli na kumbi za mikutano, huduma za
masoko na mawasiliano, maofisi na maduka pamoja na maegesho ya magari, vituo
vya ferry, maeneo ya burudani afya na michezo. Maeneo ya asili ya vijiji
vya eneo hilo vikiwemo Fumba, Bweleo, Dimani na vijiji vyengine vidogo vidogo
yataheshimiwa na kuendelezwa kwa mashauriano na wanavijiji wenyewe.
Mheshimiwa
Spika,
Katika Mkoa wa Kaskazini Unguja,
tumeshaanza Mradi wa Maendeleo ya Mji wa Kisasa Kijini – Matemwe. Mradi huu
unaendelea kutekelezwa na Kampuni ya “Penny Royal” katika maeneo ya Matemwe
Muyuni, ambapo utagharimu jumla ya Dola za Kimarekani milioni 220. Mradi huo
unajumuisha ujenzi wa Hoteli ya kimataifa yenye hadhi ya nyota tano. Aidha,
mradi huo utahusisha ujenzi wa kiwanja cha kimataifa cha gofu, chenye jumla ya
vishimo 18 na ujenzi wa nyumba za makaazi kwa watu wenye kipato cha juu ambazo
zitatumia nishati ya nguvu ya upepo. Hivi sasa Kampuni hiyo inaisaidia Serikali
katika ujenzi wa barabara yenye urefu wa km 20.2 kutoka Matemwe kupitia Kijini
kuelekea maeneo ya mradi hadi Kidoti. Ujenzi wa barabara hio unaendelea vizuri.
Mheshimiwa
Spika,
Katika eneo la Mjini Unguja, katika
kipindi hiki, Serikali imepanga kutekeleza Mradi wa Kuendeleza Hoteli ya
Bwawani na eneo linaloambatana nalo. Serikali italiendeleza eneo hilo kupitia
Muwekezaji wa Kampuni ya “Quality Group” alieshinda zabuni. Kampuni hii
inakusudia kuendeleza eneo la Bwawani kwa kujenga Hoteli ya Kisasa ya nyota
tano, majengo ya kisasa ya makaazi, majengo ya biashara, mikahawa, soko la
Kizanzibari na maegesho ya magari. Jengo la sasa la hoteli ya Bwawani
litakarabatiwa kwa ajili ya kupokea wageni mashuhuri. Uendelezaji wa eneo la
Bwawani utazingatia ipasavyo athari za Kimazingira na urithi wa kale.
SEKTA YA
BIASHARA NA VIWANDA:
Mheshimiwa
Spika,
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya Saba, yenye Muundo wa Umoja wa Kitaifa
inaendelea kuimarisha mazingira ya biashara kwa kushirikiana na sekta binafsi.
Usafirishaji wa bidhaa unaendelea kuimarika mwaka hadi mwaka. Katika mwaka 2014
tumeweza kuuza nje bidhaa zenye thamani ya TZS milioni 133,591.7 kutoka bidhaa
zenye thamani ya TZS milioni 87,799.6 mwaka 2013, sawa na ongezeko la asilimia
52.14. Usafirishaji huo umeongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na jitihada zetu
za kuimarisha uzalishaji wa zao la karafuu na mwani ambayo usafirishaji wake
ulifikia TZS milioni 103,079.2 kutoka TZS milioni 75,392.6 mwaka 2013. Hili ni
ongezeko la asilimia 77.8 ya usafirishaji wote kwa mwaka 2014. Licha ya kuwepo
kwa urari kwa bidhaa kwa usafirishaji nje, takwimu hizi zinatupa matumaini
mazuri juu ya mwenendo na ukuaji wa biashara nchini.
Kuhusu
biashara baina Zanzibar na Tanzania Bara, jumla ya bidhaa zenye thamani ya TZS
milioni 23,268.7 ziliingizwa Zanzibar kutoka Tanzania Bara mwaka 2010
ikilinganisha na bidhaa zenye thamani ya TZS milioni 64,296.4 mwaka 2014. Vile
vile, bidhaa zenye thamani ya TZS milioni 2,203.8 zilisafirishwa kwenda
Tanzania Bara mwaka 2010 ikilinganishwa na bidhaa zenye thamani ya TZS
366,354.2 mwaka 2014. Kwa jumla, katika kipindi hiki cha kwanza cha Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba, urari wa biashara kati ya Zanzibar na
Tanzania Bara unaendelea kuwa mzuri kwa upande wa Zanzibar.
Mheshimiwa
Spika,
Ni
dhahiri kuwa juhudi zilizochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya
Awamu ya Saba, za kufufua zao la Karafuu zimezaa matunda mazuri. Mpango wa
miaka kumi wa kufufua zao hili, tumekuwa tukiutekeleza kwa mafanikio. Katika
kipindi cha miaka mitatu ya kwanza ya mpango huo; 2011/12 - 2013/2014, jumla ya
tani 11,477 za karafuu zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 130.82
zilisafirishwa na kuuzwa nje ya nchi. Kiwango hicho ni sawa na ongezeko la tani
2,792 ambalo ni sawa na asilimia 32.1 ikilinganishwa na mwaka 2008/09 -
2010/2011. Hadi kufikia tarehe 12 Juni, 2015
jumla
ya tani 2, 822 zenye thamani ya TZS bilioni 39.48 zilinunuliwa kutoka kwa
wakulima.
Mheshimiwa
Spika,
Serikali
imetimiza ahadi niliyoitoa mwaka 2011 ya kuwalipa wakulima wa zao la Karafuu
asilimia 80 ya bei ya karafuu ya Soko la Dunia. Karafuu za Daraja la Kwanza
zinanunuliwa kwa bei ya TZS 14,000 kwa kilo badala ya TZS 5,000 kwa kilo, bei
iliyokuwepo mwaka 2010. Ongezeko hili ni sawa na asilimia 180. Kadhalika, vituo
vipya vya ununuzi na uuzaji wa karafuu vimejengwa Unguja na Pemba, vituo vya
zamani vimekarabatiwa na huduma zote muhimu zinapatikana kwenye vituo hivyo.
Tumefanikiwa sana katika kupambana na Magendo ya Karafuu na wananchi wanauza
Karafuu zao katika Vituo vya ZSTC. Tunawashukuru Wananchi na Vikosi vyetu vya
Ulinzi na Usalama kwa kazi nzuri, walioifanya ya kushirikiana na Serikali
katika kupambana na Magendo ya Karafuu.
Mheshimiwa
Spika,
Maamuzi
ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba, ya kulifanyia mageuzi
Shirika la ZSTC yamekuwa na manufaa makubwa kwetu. Ni habari njema kwetu sisi
viongozi na wananchi kutambua kwamba Shirika limegeuka kutoka kuendeshwa kwa
hasara kuwa Shirika lenye kuendesha shughuli zake kwa faida. Hivi sasa Shirika
linalipa kodi ya mapato na kulipa faida nyengine Serikalini. Imebainishwa kuwa
kwa hesabu zilizokaguliwa katika mwaka wa 2011/2012, 2012/2013 pamoja na
makadirio kwa hesabu za 2013/2014 Shirika limelipa jumla ya TZS 1.8 bilioni
kama kodi ya mapato na kulipa gawio la TZS milioni 500 kwa mwaka 2013/2014.
Nachukua nafasi hii kutoa pongezi kwa Uongozi na Wafanyakazi wa ZSTC kwa
mafanikio haya.
Mafanikio
yaliyopatikana katika kuliimarisha zao la karafuu, kupambana na magendo na
kulifanyia mabadiliko Shirika la ZSTC, yametokana na Ilani ya CCM ya Uchaguzi
Mkuu ya 2010/2015 ya kutolibinafsisha zao la karafuu, lakini uandaliwe mpango
madhubuti wa maendeleo ya karafuu.
Mheshimiwa
Spika,
Kwa
kutambua umuhimu wa viwanda katika kukuza uchumi na kuimarisha Soko la Ajira,
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba, ilipanga na kutekeleza
mipango mbali mbali yenye lengo la kukuza sekta ya viwanda. Ongezeko la bidhaa
zinazozalishwa viwandani katika kipindi hiki cha miaka mitano linatupa
matumaini na ari ya kuendeleza kwa kasi zaidi.
Thamani
ya bidhaa zilizozalishwa viwandani imeongezeka kutoka TZS bilioni 128 mwaka
2013 hadi kufikia TZS 136 bilioni mwaka 2014. Hili ni sawa na ongezeko la
asilimia 5.5. Wawekezaji wamekuwa wakiwekeza katika viwanda vya usafishaji
nafaka, usindakaji maziwa, uzalishaji sukari, maji ya kunywa na vinywaji mbali
mbali. Aidha, pamekuwa na ongezeko la ukuaji wa viwanda vidogo vidogo
vinavyozalishwa na wajasiriamali wanaozalisha sabuni, vifaa vya ujenzi, samani
na bidhaa za viungo Unguja na Pemba.
Ukuaji
huo vile vile umepelekea kuwepo kwa ongezeko la mchango wa sekta hii kwa Pato
la Taifa ambapo katika mwaka 2014 ulifikia asilimia 9.9 kutoka asilimia 6.9
mwaka 2013. Taasisi ya Viwango tuliyoianzisha baada ya kupitisha Sheria ya
Viwango Namba 1 ya mwaka 2011 imeanza kazi zake katika kuimarisha bidhaa
zinazozalishwa na kuingizwa nchini.
Tunaendelea
kushirikiana na sekta binafsi katika kuimarisha sekta ya Viwanda na Biashara
ikiwa ni pamoja na kuyafanyia kazi mapendekezo yanayotolewa na Baraza la
Biashara la Zanzibar (ZNBC) katika mikutano ya kila mwaka tunayoendelea
kuifanya. Natoa shukurani kwa wajumbe wa ZNBC na wale wote wanaoshiriki katika
mikutano ya mwaka ya Baraza hili kwa michango na mashirikiano wanayotoa kwa
lengo la kukuza sekta zetu muhimu za uchumi hasa Biashara, Viwanda na Utalii.
Aidha, natumai kwamba juhudi zetu za kuanzisha Tamasha la Biashara zitakuwa na
mchango mkubwa katika kutangaza na kukuza biashara, viwanda na shughuli mbali
mbali za ujasiriamali zinazoendeshwa nchini.
UTALII:
Mheshimiwa
Spika,
Katika
kipindi cha miaka mitano, tumefanikiwa sana kuiendeleza sekta ya utalii.
Tumeitekeleza kwa mafanikio dhana ya utalii kwa wote niliyoitangaza rasmi
tarehe 16 Oktoba, 2011. Serikali imeifanyia marekebisho Sheria ya utalii ya
mwaka 2009, na kupelekea kuundwa kwa Sheria mpya Namba 7 ya mwaka 2012 ambayo
inakidhi haja na kwenda sambamba na dhana ya utalii kwa wote na kutoa miongozo
imara ya kuiendesha sekta hiyo.
Takwimu
zinaonesha kuwa Idadi ya watalii 132,836 walitembelea Zanzibar katika mwaka
2010; ambapo katika mwaka 2014 watalii wapatao 311,801 waliwasili Zanzibar.
Hili ni ongezeko la asilimia 134 katika kipindi cha miaka minne. Katika
kuhakikisha usalama wa wananchi na wageni wanaotutembelea, Serikali imeandaa
Mradi wa usalama katika maeneo ya Mji wa Unguja. Jumla ya fedha kwa mradi wote
kwa kipindi cha miaka mitano ni Dola za Marekani Milioni 28.9. Fedha
zilizotengwa kwa matumizi ya mwaka wa kwanza ni TZS bilioni 10. Mradi huu
utatupatia vifaa vya CCTV, magari ya zimamoto, boti za doria na mashine ya
kukagulia vifaa vya hatari vilivyofichwa katika magari. Vifaa hivyo tayari
vimeshaagiziwa na Kampuni ya RAVITALCO ya Romania na ROM SOLUTION iliyosajiliwa
Zanzibar. Vile vile, kwa kushirikiana na Kampuni ya Mawasiliano ya ZTE ya China
tayari tumeshafunga kamera maalum za usalama (CCTV) katika maeneo ya Mji wa
Unguja. Kadhalika, kwa lengo la kuimarisha ulinzi kwa watalii, Serikali
imeanzisha Kampuni ya Ulinzi ya JKU, ambayo itatoa huduma kwa sekta binafsi
kwenye mahoteli.
Mheshimiwa
Spika,
Katika
kipindi hiki cha miaka mitano, tumeshuhudia ongezeko la wawekezaji katika
ujenzi wa hoteli za kisasa zenye hadhi ya juu. Aidha, tumeshuhudia ongezeko la
vivutio vya utalii ikiwa ni pamoja na ujenzi wa viwanja vya mchezo wa gofu
ambao unapendwa na watalii. Kumekuwa na ongezeko la idadi ya wageni wanaotoka
Mashariki ya Kati na Mashariki ya mbali baada ya kuongeza juhudi za kuitangaza
Zanzibar katika maeneo hayo mapya. Chuo cha Maendeleo ya Utalii nacho
kimeimarishwa ili kiendelee kutoa
rasilimali
watu wenye ujuzi, taaluma na stadi zinazohitajika na wawekezaji wanaokuja
nchini.
MAKUMBUSHO NA
MAMBO YA KALE:
Mheshimiwa
Spika,
Katika
kipindi cha miaka mitano, tumefanya jitihada za pamoja katika kufanya
matengenezo ya makumbusho na kuyatunza mapango mbali mbali. Serikali iko katika
hatua za mwisho za kukamilisha Sera ya Urithi wa Utamaduni itakayotoa muongozo
wa matumizi bora ya maeneo ya urithi ili kuimarisha shughuli za utalii.
Miongoni mwa maeneo ya historia, mambo ya kale na urithi wa utamaduni
tuliyoweza kuyaimarisha ni Mangapwani, Kuumbi Jambiani na Kwa Bi. Khole kwa
upande wa Unguja na Chwaka - Tumbe kwa upande wa Pemba. Natoa wito kwa wananchi
waendeleze utamaduni wa kuyatembelea maeneo yetu hayo ili kuimarisha utalii wa
ndani.
SEKTA YA KILIMO:
Mheshimiwa
Spika,
Kwa
kutambua kuwa, kilimo ndio chanzo kikuu cha ajira za wananchi kwa asilimia 70
ya ajira na kinatoa asilimia 27.3 katika Pato la Taifa, niliahidi Serikali
itafanya juhudi ya kuiendeleza sekta hii kwa kauli mbiu ya Mapinduzi ya Kilimo.
Serikali imefanya jitihada mbali mbali ili kuongeza uzalishaji wa mazao hasa
mpunga ili kuwa na uhakika wa chakula na lishe. Serikali imenunua pembejeo
mbali mbali za kilimo, imeajiri wataalamu wa ugani na imetekeleza programu
niliyoianzisha mwaka 2011 ya kuwapa ruzuku wakulima ya asilimia 75 ya gharama
za bei ya mbolea, mbegu, dawa ya magugu na huduma za matrekta.
Jitihada
hizo za Serikali ziliweza kuzaa matunda kwa kuongezeka kiwango cha uzalishaji.
Mavuno ya zao la mpunga kwa jumla yameongezeka kutoka tani 21,014 mwaka 2010
hadi tani 33,655 mwaka 2013. Hili ni sawa na ongezeko la asilimia 60. Katika
kipindi hiki Zanzibar imepata mafanikio makubwa ya uzalishaji wa mazao muhimu
ya chakula hadi kufikia tani 674,334.
Mheshimiwa
Spika,
Katika
kipindi cha miaka mitano, Serikali imefanya jitihada za kuimarisha kilimo cha
umwagiliaji maji ili kupunguza tatizo linalotukumba katika kilimo cha kutegemea
mvua zisizo za uhakika. Ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji maji wa hekta
2,200 katika mabonde ya Cheju, Kibokwa, Kilombero, Mlemele na Makwararani
umeanza kushughulikiwa kwa hatua mbali mbali.
Kadhalika,
kwa kutambua umuhimu wa utafiti katika kuleta maendeleo ya kilimo, Serikali
imefanya jitihada za kukiimarisha kituo cha utafiti wa kilimo Kizimbani kwa
kukipandisha hadhi kuwa Taasisi ya Utafiti ya Kizimbani. Taasisi hii
imeshirikiana vyema na Tume ya Sayansi na Teknolojia ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania (COSTECH) katika shughuli za utafiti. Jumla ya mbegu 43 zimefanyiwa
utafiti kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa zao la Mpunga wa Kimataifa
(IRRI). Kadhalika, Taasisi hii imefanya tafiti juu ya mbegu za mazao ya mizizi
na kutoa mbegu zinazostahamili maradhi na kunawiri katika mazingira yetu.
Katika
kuhakikisha upatikanaji wa mbegu bora za mazao mbali mbali, Serikali imekuwa
ikiendeleza majaribio ya mbegu ya mpunga ya NERICA katika vituo vya Mwera na
Kizimbani. Hivi sasa wakulima tayari wameshapatiwa mbegu hii kwa ajili ya
uzalishaji na kuiendeleza. Tafiti mbali mbali zimeonesha kuwa hii ni mbegu bora
kwa mazingira yetu kwa kuwa inastahamili ukame na inastawi hata katika ardhi
isiyo ya mabondeni.
Mheshimiwa
Spika,
Serikali
imefanya juhudi kubwa katika kuhifadhi misitu na miti yetu ya asili. Zanzibar
imejaaliwa kuwa na miti ya aina mbali mbali ya asili ambayo idadi yake imeanza
kupotea na hatukuwa na utaratibu bora wa kuitunza. Katika kukabiliana na hali
hiyo, Serikali ilifanya jitihada za kuendesha sensa ya miti mwaka 2013 ili
kujua idadi ya miti iliyopo.
Pamoja
na jitihada hizo, Serikali imeongeza juhudi za uhifadhi wa misitu yetu ya asili
ikiwa ni pamoja na msitu wa Jozani, Ufufuma, Kiwengwa na Makangale pamoja na
kusimamia
Mradi wa Hifadhi ya Misitu ya Asili (HIMA) katika maeneo mbali mbali, Unguja na
Pemba. Kwa lengo la kuongeza idadi ya miti tuliyonayo, katika kipindi hiki
jumla ya miti milioni 5 ya misitu ilioteshwa katika vitalu vya Serikali na
miche milioni 8 katika vitalu vya watu binafsi.
Jitihada
maalum zimefanywa katika kuimarisha kilimo cha karafuu, ambalo ni zao letu kuu
la uchumi. Serikali imewahamasisha wakulima wa zao hilo kuyaendeleza mashamba
yao na kuwapatia miche bila ya malipo. Hatua hiyo ni miongoni mwa utekelezaji
wa mpagno wa miaka kumi wa kulifufua zao la karafuu. Katika kipindi cha
2010-2014 jumla ya miche ya mikarafuu milioni 3.7 iligawiwa kwa wakulima katika
lengo lilokusudiwa la kutoa miche milioni 3.8.
MIFUGO NA UVUVI:
Mheshimwa Spika,
Katika
sekta ya mifugo, Serikali iliweka malengo ya kuleta mapinduzi ya ufugaji ili
kuongeza tija na ubora wa mazao yanayotokana na shughuli hiyo. Dhamira ya
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuwa na ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa
maziwa, mbuzi na kuku kwa lengo la kuongeza tija na kipato cha wafugaji wetu.
Soko la maziwa sasa limekua kutokana na muwekezaji Mzalendo (kufungua kiwanda
cha maziwa) Fumba.
Serikali
vile vile, imeimarisha maabara ya mifugo Maruhubi kwa kuifanyia matengenezo
makubwa, kuweka vifaa vya kisasa vya kuhifadhia mbegu bora za ng’ombe na
kuendeleza mradi wa upandishaji ng’ombe kwa shindano ili kupata ng’ombe bora.
Kadhalika,
Serikali iliendesha mradi wa kudhibiti maradhi ya mifugo yasiyo na mipaka
ambapo ng’ombe 20,000 walichanjwa kwa kuwakinga na maradhi ya chambavu na
kimeta na kuku 80,000 walichanjwa ili kuwakinga na mahepe.
Mheshimiwa
Spika,
Nilianzisha
Mapinduzi ya uvuvi kama nilivyotamka katika Hotuba yangu ya tarehe 11 Novemba,
2010, katika Baraza hili. Mwaka 2010 tuliahidi kufanya jitihada za kuziimarisha
shughuli za uvuvi kwa kutambua umuhimu wake katika kutoa ajira,
kutupatia
lishe bora na kuongeza mchango wake katika Pato la Taifa. Nina furaha kuwa
Serikali imepata mafanikio katika utekelezaji wa azma hiyo ambapo mchango wa
sekta hiyo katika Pato la Taifa umefikia asilimia 7.2. Jumla ya tani 148,535 za
samaki zenye thamani ya TZS bilioni 527.5 zimevuliwa hadi mwaka 2014.
Ni
jambo la kutia moyo, kuona kuwa jitihada za Serikali za kushirikiana na
wananchi katika kukabiliana na vitendo vya uvuvi haramu na kuimarisha hifadhi
ya mazingira ya bahari zimesaidia sana kuongeza kiwango cha samaki wanaovuliwa.
Jumla ya wavuvi wapatao 2,520 wamepatiwa mafunzo ya uvuvi bora yakiwemo ufugaji
wa samaki na viumbe wengine wa baharini.
Serikali
imeandaa mpango wa ujenzi wa kituo cha kutotolea vifaranga vya samaki katika
eneo la Beit - el-Ras na imetoa mafunzo kwa wafugaji wa samaki 69 kuhusu
utengenezaji wa chakula, ulishaji, uchimbaji wa mabwawa na utunzaji bora wa
samaki.
Mheshimiwa Spika,
Wakati
huo huo, zao la mwani ni miongoni mwa mazao ya baharini na kutupatia fedha za
kigeni. Jumla ya tani 51,687 za mwani mkavu zenye thamani ya TZS bilioni 187
zimesafirishwa nje ya nchi katika kipindi hiki.
Serikali
imewapatia vihori wakulima wa mwani wa Unguja na Pemba kwa ajili ya kubebea
mwani. Tunafanya juhudi kuwapa nguvu wakulima wa mwani ili kuhakikisha zao hili
linasarifiwa hapa nchini kwa lengo la kukuza uchumi wetu na kuongeza kipato cha
wakulima wetu. Aidha, kufuatia safari yangu ya China na Vietnam
niliwashajihisha wawekezaji kushiriki katika sekta hiyo. Matumaini yetu ya
utekelezaji ni mazuri.
Kwa
lengo la kuongeza mapato yanayotokana na uvuvi, Serikali imejiwekea lengo la
kuanzisha programu ya uvuvi wa bahari kuu. Programu hii inakusudiwa kuwawezesha
wavuvi wetu kuvua katika kina kirefu cha maji ili kuongeza kiwango cha samaki
wanaovuliwa na kuongeza fursa za ajira, biashara na kuchangia katika ukuaji wa
uchumi. Programu hiyo itaendeshwa kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Japan
(JICA). Maandalizi ya programu hiyo yamekwishaanza.
Mheshimiwa
Spika,
Serikali
imeandaa mpango wa kuendeleza uvuvi wa bahari kuu kwa lengo la kuwawezesha
wavuvi na vifaa kuongeza kipato chao. Serikali imefikia makubaliano na Serikali
ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) kuimarisha diko na soko
la samaki la Malindi ili liwe la kisasa na lenye uwezo wa kuhudumia vyombo vya
uvuvi ikiwemo vinavyovua bahari kuu. Utekelezaji wa mradi huo utakaogharimu
Dola za Marekani 244,500 na utaanza mwaka huu. Utakapomalizika utawanufaisha
wananchi wengi.
Kadhalika,
Serikali imewakaribisha wawekezaji kwa makubaliano ya kuwashirikisha wavuvi
wazalendo. Katika mwaka 2015, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imefikia
makubaliano ya awali na Mwekezaji (Hairu Fisheries Management Company) kutoka
Sri Lanka ya kuleta vyombo 20 vya urefu wa mita 18 ambavyo vina uwezo wa kuvua
katika kina kirefu na kukaa baharini kwa muda mrefu. Aidha, Mwekezaji huyo
atajenga Kiwanda cha Boti za Uvuvi za mita 6 na mita 9 ambazo watauziwa wavuvi
wetu.
Hatua
hizo zitaimarisha juhudi za Serikali za kuwawezesha wananchi kuitumia raslimali
ya bahari kuu kujiongezea kipato chao.
MAZINGIRA:
Mheshimiwa
Spika,
Serikali
inatambua umuhimu wa hifadhi ya mazingira katika utekelezaji wa mipango yetu
yote ya maendeleo na imechukua jitihada za kukabiliana na uharibifu wake
unaosababishwa na wanadamu na ule unaotokana na athari za mabadiliko ya tabia
nchi.
Miongoni
mwa hatua zilizochukuliwa na Serikali ni kuandaa Sera mpya ya Mazingira ya
mwaka 2013 yenye kutoa muongozo kwa shughuli za uhifadhi wa mazingira nchini na
kutayarisha Sheria mpya ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2015.
Serikali
imezingatia haja ya kufanya tathmini ya athari za mazingira katika miradi ya
uwekezaji ambapo jumla ya tathmini 71 za athari za mazingira zimefanywa na
wahusika kupewa vyeti. Kadhalika, miradi 221 imefanyiwa ufuatiliaji wa
kimazingira na kutolewa ushauri. Vile vile, Serikali imechukua hatua za
kukabiliana na athari za tabia nchi.
Mheshimiwa
Spika,
Mnamo
mwezi Septemba, mwaka 2014 nilihudhuria mkutano wa nchi ndogo za visiwa
zinazoendelea nchini Samoa, kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Tanzania ilipata heshima ya
kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa mkutano na nikapewa heshima ya kuhutubia
kikao cha ufunguzi uliofanywa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Ban ki
Moon.
Tukio
moja wapo muhimu wakati wa mkutano huo ni uzinduzi wa Mpango wa Magharibi ya
Bahari ya Hindi wa changamoto za Ukanda wa Pwani na Mabadiliko ya Tabianchi
(Western Indian Ocean Coastal Challenge (WIOCC). Visiwa vinavyoshiriki mpango
huo ni pamoja na Sychelles, Comoro, Mauritius, Reunion na Zanzibar. Uzinduzi
huo ulihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa nchi za visiwa pamoja na Washirika
wa Maendeleo wakiwemo Island Partnership (GLISPA).
VYAMA VYA
USHIRIKA NA SACCOS:
Mheshimiwa
Spika,
Wananchi
wamefaidika na taasisi hizo kwa kujipatia ajira na mikopo ya kujiendeleza. Ili
kukuza taaluma ya vyama vya ushirika na SACCOS zilizopo, Serikali imeandaa
mpango mkuu wa mafunzo wa miaka mitatu (Training Master Plan), pamoja na
kuandaa miongozo ya aina 13 ya kufundishia kwa mujibu wa mahitaji ya mafunzo
yaliyoibuliwa.
KAZI, AJIRA NA
UTUMISHI WA UMMA:
Mheshimiwa
Spika,
Katika
kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana na wanawake na kuwajengea
uezo wa kipato wananchi, katika kipindi hiki cha miaka mitano Serikali
imeanzisha
Mfuko wa Uwezeshaji hapo tarehe 21 Disemba, 2013 ukiwa na jumla ya fedha TZS
bilioni 2.413, baada ya kuunganishwa Mfuko wa Kujitegemea, Mfuko wa JK na AK na
Mfuko wa Vijana. Kati ya fedha hizo, TZS milioni 973 zilipatikana kwa
kuchangishwa kupitia Kamati niliyoiunda, TZS bilioni 1.2 zilitokana na mfuko wa
AK/JK na jumla ya TZS milioni 140 ni za Mfuko wa Rais wa Kujitegemea na TZS
milioni 100 zilitokana na Mfuko wa Vijana. Lengo kuu kuunda Mfuko wa
Kujitegemea ni kuwa na Mfuko ulio imara zaidi katika kuwasaidia vijana,
wanawake na vikundi mbali mbali vya wajasiriamali katika shughuli zao za
kujiendeleza kiuchumi.
Katika
kuhakikisha kuwa vijana wanapata fursa za ajira, tumefanikiwa kuzindua Mpango
Mkakati wa Ajira kwa vijana wa mwaka 2014/2018. Mpango huu umeweka vipaumbele
katika sekta za ujasiriamali, elimu ya amali pamoja na ufundi stadi. Tumepata
mafanikio katika kutekeleza Programu ya Ajira kwa vijana katika sekta ya kilimo
kupitia mashamba darasa, shughuli za uvuvi, ufugaji na utalii. Nachukua fursa
hii kuwapongeza vijana na wanawake kwa ari na moyo walioonesha katika kuunga
mkono jitihada hizi na kwa kutumia vizuri fursa tulizowaandalia.
Mheshimiwa
Spika,
Katika
kipindi hiki cha miaka mitano tumefanikisha kupatikana kwa nafasi za ajira
25,019 Serikalini na katika Sekta Binafsi. Kati ya hizo, nafasi za ajira 4,850
zilikuwa za taasisi mbali mbali za Serikali na nafasi za ajira 20,169
zilitokana na sekta binafsi, zikijumuisha ajira za nje ya nchi na taasisi
zinazojitegemea kwa wananchi wa Zanzibar wenye sifa zilizohitajika. Ajira bado
ni changamoto nchini kwetu na katika nchi za nje hata zile zilizoendelea. Kwa
kiasi kikubwa tumefanikiwa kupambana na tatizo hilo na mipango yetu chini ya
mkakati wa ajira unatoa matumaini mazuri.
Mheshimiwa
Spika,
Wakati
huo huo, Serikali imefanikiwa kupandisha mishahara ya watumishi wa umma kutoka
kima cha chini cha mshahara wa Tsh.100,000 hadi TZS 125,000 kwa mwezi sawa na
asilimia ishirini na tano (25%) pamoja na kufanya marekebisho ya mishahara ya
wataalamu na wafanyakazi mbali mbali wakiwemo Madaktari, Walimu wa Sayansi na
kadhalika. Serikali ilifanya marekebisho hayo ya mwanzo katika mwaka 2011.
Vile
vile, mwishoni mwa mwaka 2013 na mwanzoni mwa mwaka 2014, Serikali ilipandisha
kima cha chini cha mshahara kutoka TZS 125,000 hadi TZS 150,000 sawa na
asilimia ishirini (20%) pamoja na kurekebisha mishahara ya watumishi wazoefu,
waliotumikia katika utumishi wa umma kwa miaka kumi na tano (15) na zaidi ambao
wana mishahara kati ya TZS 150,000 hadi TZS 225,000 katika jitihada za
kunyanyua kipato cha mfanyakazi, Serikali imeidhinisha posho mbali mbali ambazo
tayari zimeanza kutolewa. Malimbikizo ya mishahara ya walimu yatalipwa kutoka
bajeti ya mwaka wa fedha wa 2015/2016 iliyopitishwa na Baraza hili.
MIUNDO YA
UTUMISHI:
Mheshimiwa
Spika,
Katika
kuimarisha utendaji kazi, Serikali imerudisha tena utaratibu wa kuwa na Miundo
ya Utumishi katika Mawizara na Taasisi mbali mbali za Serikali. Wizara zote
tayari zimeshatengeneza Miundo yao ya Utumishi na zimewasilishwa katika
Kamisheni ya Utumishi wa Umma kwa kuthibitishwa. Taasisi nyengine za Serikali
yakiwemo mashirika na taasisi zinazojitegemea zimo katika hatua za utayarishaji
wa Miundo yao ya Utumishi kwa kushirikiana na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais,
Kazi na Utumishi wa Umma. Serikali imetoa miongozo mbali mbali kwa ajili ya
kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza katika marekebisho ya mishahara na maposho
ili kuhakikisha kwamba hakuna mfanyakazi atakayedhulumiwa haki yake.
Mheshimiwa
Spika,
Vile
vile, katika kipindi cha miaka mitano, Serikali imeimarisha maslahi ya wananchi
wanaofanyakazi katika sekta Binafsi kwa kuitaka iongeze mishahara na posho za
wafanyakazi wao. Wafanyakazi wa sekta hiyo wameongezewa kiwango cha mishahara
yao kutoka TZS 70,000 mwaka 2010 hadi 145,000 kwa sasa, sawa na ongezeko la
asilimia 107.
Mheshimiwa
Spika,
Natumia
fursa hili kulipongeza Baraza lako Tukufu kwa kupitisha Sheria Namba 2 ya
Utumishi wa Umma ya mwaka 2011. Sheria hii imetuwezesha kuweka Miundo imara ya
uendeshaji na usimamizi wa Utumishi wa Umma na mambo mengine yanayohusiana na
hayo.
Kutokana
na sheria hii, Serikali imeunda Kamisheni ya Utumishi wa Umma pamoja na Tume ya
Utumishi Serikalini, Tume ya Utumishi ya Mahakama, Tume ya Utumishi ya Baraza
la Wawakilishi na Tume ya Utumishi ya Idara Maalum. Taasisi hizi ni muhimu
katika kulinda maslahi na haki za wafanyakazi hapa nchini na zimetoa mchango
mkubwa katika kuweka misingi mikuu ya maadili ya Utumishi wa Umma na usimamizi
wa rasilimali watu.
Jumla
ya Sheria za kazi 12 zimetungwa na zimeanza kutumika, zikiwemo kanuni za mwaka
2014 za Sheria ya Utumishi wa Umma Nambari 2 ya mwaka 2011. Haya yote ni
mafanikio ya utekelezaji wa ahadi nilizozitoa za kulinda na kukuza maslahi ya
wafanyakazi Serikalini na katika Sekta Binafsi.
Mheshimiwa
Spika,
Katika
kuimarisha ustawi wa kinamama na watoto, kuanzia tarehe 21 Aprili 2015
tulianzisha utaratibu unaowawezesha akina mama wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii (ZSSF), kulipwa mafao ya uzazi wanapokwenda kujifungua ili yawasaidie
kuimarisha afya zao na za watoto katika kipindi hicho muhimu. Malipo ya mafao
ya uzazi hayaathiri malipo ya mafao, ambayo muhusika atapata wakati
atakapostaafu.
Mheshimiwa
Spika,
Tunamaliza
miaka mitano ikiwa tumo katika hatua za mwisho za kukamilisha Sera ya Usalama
na Afya Kazini ili kuweka mfumo mzuri wa afya katika maeneo ya kazi kwa lengo
la kuwakinga wafanyakazi na ajali na majanga mengine yanayotokea katika sehemu
za kazi. Aidha, tunamaliza kipindi hiki ikiwa tupo katika hatua za kuanzisha
Bima ya Afya. Tumeshafikia hatua nzuri katika kuifikia azma hiyo.
SEKTA YA
MIUNDOMBINU:
Mheshimiwa
Spika,
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba ilitambua kuwa lengo lake la kukuza
uchumi wa Zanzibar halitaweza kufanikiwa bila ya azma hiyo kwenda sambamba na
uimarishaji wa miundo mbinu ya uchumi kama vile barabara, bandari, viwanja vya
ndege, kuimarisha maeneo huru ya uwekezaji pamoja na kuwa na nishati ya uhakika
ya umeme. Kwa hivyo, katika kipindi hiki cha miaka mitano, jitihada kubwa
zimefanywa katika kuimarisha miundo mbinu hiyo ya uchumi.
Mheshimiwa
Spika,
Kuhusu
miundo mbinu ya barabara, Serikali imeendeleza na imekamilisha kazi za ujenzi
wa barabara zote kuu zinazoingia mjini. Kadhalika, tumeweza kujenga barabara
ndogo ndogo za mijini na mashamba na kuifanya Zanzibar kuwa mfano wa nchi zenye
mtandao mzuri wa barabara unaounganisha miji na mashamba na kuwa ni kichocheo
muhimu cha maendeleo ya uchumi na kurahisisha shughuli za usafiri wa wananchi
na mizigo.
Mheshimiwa
Spika,
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba, imekamilisha kazi ya ujenzi wa barabara
11 zenye urefu wa (km 102) katika Kisiwa cha Pemba na barabara 4 zenye urefu wa
km 34.85 katika Kisiwa cha Unguja. Barabara hizi zimejengwa kwa msaada wa MCC
ya Marekani, BADEA na Saud Fund na SMZ. Hivi karibuni tunatarajia kufanya
uzinduzi wa barabara ya Wete hadi Gando (km 15) na barabara ya Wete hadi Konde
(km 15), ujenzi ambao utakuwa ni suluhisho la tatizo la barabara la muda mrefu
lililokuwa likiwasumbuwa wananchi wanaoishi katika maeneo mbali mbali.
Kadhalika, kupitia Mfuko wa Barabara Serikali ilikamilisha ujenzi wa barabara
ya Amani hadi Mtoni (km 4) na barabara ya njia nne hadi Umbuji yenye urefu wa
(km 5). Kazi ya ujenzi wa barabara ya Jendele, kupitia Cheju hadi Unguja Ukuu
(km 11.7) na barabara ya Koani hadi Jumbi (km 6.3) kwa msaada wa BADEA
unaendelea. Kadhalika, ujenzi wa barabara ya Ole hadi Kengeja yenye urefu wa
(km 35) inayojengwa kwa msaada wa
OPEC
Fund umeshaanza na ujenzi wa barabara kuu kutoka Chake chake hadi Wete
unatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Mheshimiwa
Spika,
Uimarishaji
wa usafiri wa anga ni miongoni mwa masuala yaliyozingatiwa na Serikali ya Awamu
ya Saba kama nilivyoahidi wakati wa uzinduzi wa Baraza hili mwaka 2010.
Jitihada kubwa zimefanywa katika kukamilisha kazi ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ikiwa ni pamoja na ya kurukia ndege,
maegesho ya ndege, ujenzi wa uzio, sehemu ya kuegesha magari, ujenzi wa jengo
la abiria na kuimarisha huduma mbali mbali zinazohusiana na matumizi ya uwanja
huo. Ujenzi wa njia ya kurukia ndege na sehemu ya kuegesha ndege imekamilika na
ujenzi wa jengo jipya la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid
Amani Karume umefikia hatua nzuri ya utekelezaji.
Mheshimiwa
Spika,
Kuhusu
kiwanja cha ndege cha Pemba, Serikali inaendeleza mipango mbali mbali kwa ajili
ya kukiimarisha kiwanja hiki ili kiweze kutumika usiku na mchana na baadae
kiweze kutumiwa na ndege zilizo kubwa zaidi.
Katika
juhudi tunazoendelea kuchukua za kuimarisha kiwanja hicho, tarehe 16 Machi 2015
Serikali iliingia mkataba na Kampuni ya Safegate ya Ujerumani kwa ajili ya
uletaji wa vifaa pamoja na kusimamia uwekaji wa taa katika kiwanja kwa gharama
ya Dola za Kimarekani 508,219.45. Hivi sasa, Kampuni ya hiyo imeshalipwa malipo
ya awali ya aslimia 20.
Vifaa
mbali mbali kwa ajili ya uwekaji taa hizo vimeshafika Pemba na kazi ya
uchimbaji misingi kwa ajili ya kulaza nyaya imeanza. Kwa upande wa usimamizi wa
“civil work” mtaalamu wa Kampuni hiyo tayari amewasili katika kiwanja cha ndege
cha Pemba kusimamia kazi ya uchimbaji misingi na mashimo. Kazi ya uwekaji taa
inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi wa Julai.
Sambamba
na juhudi hizi Serikali, inaendelea kufanya mazungumzo na washirika wa
maendeleo mbali mbali ili kupata fedha kwa ajili ya kuimarisha zaidi Uwanja wa
Ndege wa Pemba. Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imekubali kufadhili kazi ya
Upembuzi Yakinufu na mpango mkuu wa kiwanja hicho; kazi ambayo inatarajiwa
kuanza ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo. Kukamilika kwa mradi huu
kutasaidia sana katika jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali za
kuitangaza Pemba katika masoko ya utalii duniani na kuimarisha biashara na
huduma za usafiri kwa wananchi wa Unguja na Pemba.
Mheshimiwa
Spika,
Serikali
imezingatia umuhimu wa bandari, kwa hivyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Azam
Marine imejenga majengo mapya ya kupumzikia abiria katika Bandari ya Malindi.
Aidha, vifaa mbali mbali vimenunuliwa ili kuongeza ufanisi na kasi ya upakiaji
na uteremshaji wa mizigo katika meli zinazofika Bandari ya Malindi. Serikali
vile vile imeifanyia matengenezo makubwa gati ya Mkoani Pemba ili kurahisisha
shughuli za usafiri wa vyombo na abiria wanaoitumia bandari hiyo.
Ujenzi
wa gati ya Tumbatu unaendelea na ujenzi wa gati ndogo ya Mkokotoni unategemewa
kuanza katika mwaka wa fedha, 2015/2016. Katika kukabiliana na tatizo la uhaba
wa nafasi katika Bandari ya Malindi na kuwa na Bandari ya kisasa yenye huduma
bora zaidi, tayari Serikali imeanza hatua za awali za ujenzi wa Bandari mpya ya
Mpiga duri. Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imekubali kushirikiana nasi
katika ujenzi huo kupitia Benki ya Exim ambapo hatua ya Upembuzi Yakinifu
zimeshafanywa na Kampuni ya Chec ya China ndio itakayojenga bandari hio kwa
kushirikiana na Serikali.
Mheshimiwa
Spika,
Tumefikia
hatua nzuri katika kutekeleza Ujenzi wa bandari hiyo ambao ulibuniwa kabla ya
mwaka 2000. Serikali imepanga kujenga Bandari hiyo kubwa na ya kisasa ili
Zanzibar iweze kwenda sambamba na mabadiliko ya biashara na uchumi yanayotokea
duniani. Bandari hii mpya itahudumia meli zenye uzito wa Tani 50, 000
(Deadweight tonnage) na itakuwa na urefu wa mita 300 na upana wa mita 490.
Ujenzi wa bandari hio
utaanza
mara tu baada ya kukamilika kwa ujenzi wa jengo jipya la abiria la Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (Terminal 2).
Kwa
lengo la kuimarisha usafiri wa baharini, Serikali iliamua kujenga Meli ya
abiria na mizigo ili kupunguza tatizo kwa wananchi na wafanyabiashara. Meli
hiyo inayojengwa katika Jamhuri ya Korea inayotarajiwa kufika nchini katika
mwezi wa Julai, 2015 ina uwezo wa kuchukua abiria 1,200 na mizigo yenye uzito
wa tani 200.
Mheshimiwa
Spika,
Nishati
ya umeme ni muhimu katika kuimarisha ukuaji wa uchumi wa nchi na ustawi wa
maendeleo ya wananchi wetu. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika awamu zake
mbali mbali imefanya jitihada kadhaa za kuhakikisha Zanzibar inakuwa na huduma
ya nishati ya umeme ya uhakika. Katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba, tumeweza kukamilisha hatua hizo
zilizoanzishwa na Awamu ya sita za kuwa na umeme wa MW 100 kwa Unguja na MW 20
kwa Pemba, viwango ambavyo ni zaidi ya mahitaji halisi ya nishati hiyo kwa
sasa.
Katika
hotuba ya tarehe 11 Novemba, 2010 nilipolizinduwa Baraza la nane, niliahidi
kuwa Serikali itapeleka umeme katika maeneo yote ambayo bado hayajapata nishati
hiyo ikiwa ni pamoja na kisiwa cha Makoongwe, Kisiwa Panza na Kisiwa cha
Shamiani huko Pemba. Utekelezaji wa azma hii umefikia hatua ya kuridhisha. Nina
furaha kuelezea mafanikio makubwa ambayo Serikali imeyapata katika utekelezaji
wa usambazaji wa umeme. Hivi sasa huduma za umeme zinapatikana katika miji yote
na zimefikia zaidi ya vijiji 129 badala 123 vilivyokadiriwa mwanzo.
UCHIMBAJI WA
MAFUTA NA GESI:
Mheshimiwa
Spika,
Nimefurahi
kuona kuwa Baraza hili la Nane limejadili kwa kina suala la uchimbaji wa mafuta
na gesi na mmeweza kutoa michango na kuishauri Serikali kwa namna mbali mbali
kuhusiana na suala hili. Hivi sasa tumefikia pazuri hasa tukizingatia kuwa
Katiba Inayopendekezwa imezingatia matakwa ya Zanzibar juu ya suala hili.
Katika kipindi cha miaka mitano, Serikali imefanya mazungumzo na kusaini
makubaliano ya Awali na
Kampuni
zinajishughulisha na uchimbaji mafuta, ikiwemo Kampuni ya RAK Gas ya Ras Al
Khaima kufuatia ziara yangu ya mwaka 2012 na kampuni ya Shell kufuatia ziara ya
Uholanzi niliyoifanya mwezi Agosti, 2013. Dhamira yetu ni kuona kuwa katika
kipindi kifupi kijacho mafuta na gesi yanachimbwa Zanzibar baada ya kufanyiwa
kazi masuala ya kisheria.
HUDUMA ZA JAMII:
Mheshimiwa
Spika,
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba, ilitambua wazi kuwa kuimarisha huduma
za jamii ni jukumu lake la msingi na hatua muhimu ya kuendeleza shabaha ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964. Katika kutekeleza
azma hiyo, Serikali imechukua jitihada mbali mbali katika kuimarisha
upatikanaji wa huduma bora za Elimu, Afya na Maji Safi na Salama katika maeneo
yote ya Unguja na Pemba, mijini na mashamba.
Mheshimiwa
Spika,
Kwa
upande wa sekta ya elimu, niliahidi kuendeleza mafanikio ya elimu
yaliyopatikana katika Awamu zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
zilizotangulia. Kadhalika, Serikali yangu iliweka azma ya kuimarisha ubora wa
elimu inayotolewa katika ngazi zote kuanzia Maandalizi, Msingi, Sekondari,
Elimu ya Juu pamoja na Mafunzo ya Elimu Amali na Elimu Mbadala. Pamoja na hatua
hizo, tulidhamiria kuimarisha masomo ya sayansi hasa kwa watoto wa kike,
mafunzo ya elimu maalum kwa watu wenye ulemavu, kuimarisha maslahi ya walimu
pamoja na kuyaimarisha mazingira ya kusomea yakiwemo majengo na vifaa vya
maabara na vitabu vya kiada na ziada.
Mheshimiwa
Spika,
Ni
jambo la kufurahisha kuona mafanikio makubwa ambayo Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Awamu ya Saba, imeweza kuyapata katika utekelezaji wa malengo hayo
niliyoyabainisha ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2010 –
2015 na mipango mingine ya Kitaifa niliyoitaja hapo awali.
Wakati
tukiwa katika mwaka wa tano wa uongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
Awamu ya Saba, tunafarajika kwa mafanikio ya kuandikisha watoto wote waliofikia
umri wa kusoma. Serikali imeondoa michango ya wazazi katika elimu ya msingi na
kuondoa gharama za mitihani yote ya Sekondari kuanzia mwaka wa fedha 2015/2016
ili kuwawezesha watoto wote kupata elimu bila ya malipo kwa shabaha ile ile ya
tamko la Mwasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume
alilolitangaza tarehe 23 Septemba, 1964. Katika kipindi hiki cha miaka mitano,
tunajivunia kuongezeka kwa uandikishaji wa wanafunzi katika ngazi ya elimu ya
lazima; Maandalizi, Msingi na Sekondari kutoka jumla ya wanafunzi 317,278 mwaka
2010 hadi kufikia wanafunzi 390,464 mwaka 2015.
Mheshimiwa
Spika,
Serikali
imepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa mradi wa uimarishaji wa elimu ya
lazima kwa kutumia fedha zetu na michango ya washirika wa maendeleo kwa kujenga
majengo mapya ya skuli, kununua vifaa vya maabara na samani. Serikali imeweza kushirikiana
vyema na wananchi pamoja na sekta binafsi katika kuongeza nafasi na fursa za
kupata elimu kwa watoto wa Zanzibar na kupanua wigo wa mafunzo yanayotolewa
katika elimu ya juu hususan katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).
Kadhalika, Serikali iliendelea kuchukua hatua ya kuwapatia mikopo vijana
wanaojiunga na taasisi za elimu ya juu kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu,
Zanzibar.
Idadi
ya skuli zimeongezeka. Skuli za maandalizi sasa ni 270 kutoka 238 mwaka 2010.
Skuli za msingi zimeongezeka kutoka 299 mwaka 2010 hadi skuli 370 mwaka 2015.
Serikali inajiandaa kujenga skuli mpya 10 za ghorofa ili kuongeza nafasi kwa
wanafunzi. Ili kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia, Serikali
inatekeleza mradi wa Tz – 21 unaohusiana na masomo ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano katika skuli za msingi 248. Skuli hizo zimepatiwa vifaa mbali mbali
ikiwa ni pamoja na Kompyuta, Vitabu na Vifaa vyengine vya ufundi wa TEHAMA
pamoja na kuwapatia mafunzo watendaji wanaosimamia mradi huo.
Mheshimiwa
Spika,
Katika
hotuba yangu ya uzinduzi wa Baraza hili, niliahidi kuchukua hatua madhubuti za
kuimarisha Elimu ya Sekondari kwa kuchukua hatua mbali mbali ikiwa ni pamoja na
kuyaimarisha mazingira ya ufundishaji na usomaji kwa kuwapatia walimu mafunzo,
kujenga Skuli mpya 21 ili kuongeza nafasi, kuzifanyia matengenezo makubwa skuli
sita za sekondari na kuzipatia vitabu na vifaa vya maabara skuli zetu pamoja na
samani. Kadhalika, kwa lengo la kuwashajihisha watoto wa kike kusoma masomo ya
sayansi, niliahidi kuanzisha skuli maalum za sekondari kwa ajili ya watoto wa
kike, ambapo skuli ya sekondari ya Ben Bella kwa Unguja na skuli ya Utaani kwa
Pemba tayari zimeshaanzishwa kwa lengo hilo.
Idadi
ya Skuli za Sekondari kuanzia kidatu cha kwanza hadi cha Sita imeongezeka
kutoka skuli 194 mwaka 2010 hadi skuli 263 mwaka 2015. Serikali imeweza kukamilisha
azma yake ya kuzifanyia matengenezo makubwa Skuli sita za zamani za Sekondari
za Unguja na Pemba na kuzipatia vifaa vya maabara na samani kama ilivyoahidiwa.
Aidha, tumeweza kukamilisha ujenzi wa Skuli mpya za Sekondari 19 kama
tulivyoahidi na tayari skuli hizo zinatumika.
Serikali
imechukua jitihada maalum katika kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalum
wanapata haki yao ya elimu katika skuli zetu mbali mbali, kupitia mpango wa
elimu mjumuisho, pamoja na kuyaimarisha mafunzo ya elimu ya amali na ufundi
katika vituo vya Mwanakwerekwe, Mkokotoni na Vitongoji. Vituo hivi vimetoa
mchango mkubwa wa kuwapatia vijana wetu mafunzo mbali mbali ya fani za ufundi
zikiwemo uashi, useremala, ushoni, uhunzi, upishi, uchoraji, ufundi bomba,
ufundi umeme, magari, mafriji, teknolojia ya habari na fani nyenginezo.
Mheshimiwa
Spika,
Mafanikio
makubwa yamepatikana katika kuimarisha fursa za elimu ya juu nchini ili kwenda
sambamba na mahitaji ya wataalamu wetu wenyewe. Wanafunzi waliojiunga katika
vyuo vikuu vitatu vya Zanzibar; imeongezeka kutoka vijana 3,624 mwaka 2010 na
kufikia 6,367 mwaka 2015. Mafanikio hayo ni pamoja na ongezeko la masomo katika
viwango mbali mbali kuanzia Ngazi ya Cheti hadi Shahada ya Uzamivu (PhD).
Katika
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) katika kipindi hiki, idadi ya skuli za
masomo (faculties) imeongezeka kutoka moja hadi tano. Kadhalika, chuo hiki
tayari kimeanza benchi ya pili ya Shahada ya Uzamivu ya Kiswahili pamoja na
kuanzisha kitivo cha masomo ya udaktari (Faculty of Medicine) katika mwaka
2013. Jambo kubwa zaidi ni ongezeko la wasichana katika masomo ya juu. Katika
Mahafali ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) mwaka 2014, idadi ya
wahitimu wa kike ilikuwa ni asilimia 64 kati ya wahitimu 741 wa chuo hicho.
Mwaka huu wa 2015 chuo kina wanafunzi 2705 ambapo 1654 ni wanawake na 1051 ni
wanaume. Hayo ni miongoni mwa mafanikio ambayo nchi yetu inapaswa kuyaendeleza.
Mheshimiwa
Spika,
Kwa
lengo la kuhakikisha wanafunzi wanaopata fursa ya elimu ya juu wanaendelea na
masomo yao, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatoa mikopo kila mwaka kwa
wanafunzi wapya na wale wanaoendelea. Hadi kufikia mwezi Disemba, 2014
wanafunzi 4,678 walipewa mikopo yenye thamani ya TZS bilioni 19.4. Katika mwaka
wa fedha 2014/2015. Serikali ilipanga kutoa udhamini kwa wanafunzi wapya wa
elimu ya juu 1,200. Hata hivyo, idadi halisi iliongezeka hadi kufikia wanafunzi
1,611 sawa na ongezeko la asilimia 34 ya malengo.
Mheshimiwa
Spika,
Uimarishaji
wa huduma za afya nchini ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ya Mapinduzi,
Awamu ya Saba na Shabaha ya Mapinduzi ya mwaka 1964. Miongoni mwa jukumu la
msingi la Serikali lilikuwa ni kuyaendeleza mafanikio ya Sekta ya Afya ya Awamu
za Serikali zilizopita na kutekeleza mikakati ya mipango ya Kitaifa kupitia
Ilani ya Uchaguzi ya CCM, MKUZA II, Dira ya 2020 na Malengo ya Milenia pamoja
na kuhakikisha Sera ya Afya inatekelezwa kwa vitendo kwa kushirikiana na
wananchi.
Miongoni
mwa malengo makuu ya Serikali yalikuwa ni kuimarisha huduma za Hospitali Kuu ya
Mnazi Mmoja ili ifikie kuwa Hospitali ya Rufaa, kuiimarisha Hospitali ya
Abdalla Mzee na Hospitali ya Wete ili zifikie hadhi ya kuwa Hospitali za Mkoa.
Kwa upande wa Hospitali ya “Cottage” ya Kivunge na Makunduchi kwa Unguja na
Micheweni na Vitongoji kwa Pemba, Serikali ilikusudia zifikie hadhi ya
Hospitali za Wilaya. Hospitali ya
Koteji
ya Makunduchi imepiga hatua mbele zaidi. Malengo mengine ni kuanzisha Vitengo
vya matatizo ya Figo, Maradhi ya Moyo na Saratani ili huduma hizo ziweze
kupatikana nchini pamoja na kuziimarisha huduma za kinga na tiba.
Mheshimiwa
Spika,
Mabadiliko
makubwa yamefanywa katika kipindi cha miaka mitano katika kuimarisha mazingira
na huduma zinazotolewa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ili ifikie hadhi ya
Hospitali ya Rufaa. Hatua zilizochukuliwa na Serikali ni pamoja na kuipatia
Hospitali hiyo vifaa vya kisasa katika Chumba cha Upasuaji, Maabara ya
Uchunguzi wa maradhi, Wodi ya Wagonjwa Mahatuti, Wodi ya Wazazi na Chumba cha
Wagonjwa wa dharura. Jengo jipya la huduma za upasuaji wa Kichwa na Uti wa
Mgongo limefunguliwa likiwa ni la huduma za aina yake katika Afrika ya
Mashariki. Kituo cha Meno cha Tabasam kwa ajili ya kuwahudumia watu wenye
matatizo ya midomo nacho kimeanzishwa.
Vile
vile, Serikali imeanzisha Kitengo cha uchunguzi wa maradhi ya mfumo wa chakula
pamoja na Wodi mpya ya Wagonjwa Mahututi. Hivi sasa, Serikali inaendelea na
mradi wa ujenzi wa jengo jipya la watoto ambalo pia litakuwa na huduma za
wagonjwa wa maradhi ya figo. Ni jambo lililo wazi kuwa huduma katika Hospitali
ya Mnazi Mmoja zimeimarika sana na zimepunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya
wagonjwa ambao walikua wakifuata baadhi ya huduma nje ya Zanzibar.
Mheshimiwa
Spika,
Serikali
inaendelea na ujenzi mkubwa wa Hospitali ya Abdalla Mzee kwa kuiwekea miundo
mbinu ya kisasa na vifaa ili iweze kukidhi kuwa Hospitali ya Rufaa Pemba.
Katika Hospitali ya Wete, huduma zimeimarishwa za shughuli za uchunguzi wa
maradhi mbali mbali, ujenzi wa jengo la maabara mpya umekamilika. Wodi mpya ya wazazi,
wodi ya wagonjwa wa akili na chumba cha upasuaji zimejengwa.
Mheshimiwa
Spika,
Mwamko
wa wananchi juu ya elimu ya afya na jitihada za Serikali katika kuimarisha
huduma hizo kumechangia sana katika kuongezeka kwa asilimia ya mama waja wazito
wanaojifungua
katika vituo vya afya hadi kufikia asilimia 68.3 mwaka 2014. Hivi sasa huduma
za kujifungua zinapatikana bure katika vituo 41 nchini.
Vifo
vya watoto wanaozaliwa hai chini ya umri wa mwaka mmoja vimepungua kutoka
54/1000 mwaka 2010 hadi 46/1000 mwaka 2012 zaidi ya lengo lililokuwepo la vifo
48/1000. Vile vile kuna mafanikio katika kupunguza vifo kwa watoto chini ya
umri wa miaka 5 kutoka 73/1000 mwaka 2010, 66/1000 mwaka 2012. Lengo ni kufikia
50/1000. Vifo vya kinamama kutokana na uzazi vinazidi kupungua.
Kadhalika,
Serikali imeendelea kudhibiti kiwango cha Malaria na VVU/UKIMWI kuwa chini ya
asilimia moja. Kwa mujibu wa tathmini ya kiwango cha maambukizo ya VVU,
Zanzibar inakisiwa kuwa na asilimia 0.5 ya maambukizi kwa watu wenye umri kati
ya miaka 15 hadi 24, asilimia 0.6 kwa wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49.
Katika
kipindi hiki Serikali imejenga ghala la kisasa la kuhifadhia dawa katika eneo
la Maruhubi. Serikali za Marekani na Denmark zimesaidia ujenzi huu. Vile vile,
Ofisi ya Mkemia Mkuu hivi sasa imehamishiwa katika eneo hilo ili kupata fursa
ya kufanya shughuli zake katika mazingira yaliyo bora zaidi.
Mheshimiwa
Spika,
Jitihada
kubwa zimefanywa katika kukiimarisha Chuo cha Taaluma ya Sayansi za afya.
Mafanikio yamepatikana ambapo kwa sasa idadi ya madaktari wazalendo imefikia
102. Tunategemea idadi hiyo itaongezeka hasa baada ya Serikali kuamua kuanzisha
mafunzo ya udaktari katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na
wanafunzi wanaosomea udaktari Tanzania Bara na nje ya nchi. Kwa wastani daktari
mmoja alikuwa akihudumia wagonjwa 31,838 (1:31,838) mwaka 2010 na ambapo sasa
anahudumia wastani wa wagonjwa 18,810 (1:18,810). Pamoja na madaktari
wazalendo, wapo madaktari wa kigeni 20 kutoka China na 20 kutoka Cuba. Idadi
hii inafanya madaktari wote kuwa 151 ambapo wastani wa daktari mmoja anahudumia
watu 9,093 (1:9,093).
Napenda
nitoe shukurani zangu kwa washirika wetu wa maendeleo wanaotuunga mkono katika
azma yetu ya kuziimarisha huduma za afya nchini. Tunathamini sana misaada yao
ya mafunzo na utaalamu, vifaa, wafanyakazi na nyenzo mbali mbali ambazo kwa
pamoja zimeweza kutuletea mafanikio tuliyoyapata. Zanzibar ina mtandao mzuri wa
huduma za afya zinazotolewa katika hospitali na vituo vya afya vya Serikali,
Vikosi vya Ulinzi, Taasisi za Kijamii na vituo vya watu binafsi kuliko nchi
nyingi. Katika Bara la Afrika; mwananchi wa Zanzibar hatembei umbali wa
kilomita tano, bila ya kupata huduma za afya kwenye kituo cha afya.
MAJI SAFI NA
SALAMA:
Mheshimiwa
Spika,
Wakati
nikilifungua Baraza hili, nilisema kuwa maji ni uhai na hasa maji safi na
salama. Kwa hivyo, Serikali yangu imeendeleza jitihada za Serikali za Awamu
zilizopita na kuweka mikakati mipya katika kuwapatia wananchi huduma za maji
safi na salama. Mipango ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba, ni
pamoja na kukamilisha mradi wa usambazaji wa maji katika Mkoa wa Mjini Magharibi,
kupunguza upotevu wa maji na kuvihifadhi vianzio vya maji.
Katika
ahadi zangu nilibainisha kuwa kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka
2010 – 2015, Serikali inakusudia kusambaza huduma za maji safi na salama
kufikia asilimia 95 kutoka asilimia 75 katika miji na asilimia 80 kutoka
asilimia 60 katika vijiji ifikapo mwaka 2015. Hali ya uzalishaji wa maji
imefikia lita milioni 17.6 ambayo imewezesha kuongezeka kwa watu wanaopata maji
na kufikia 175,873 katika kipindi hiki. Mahitaji yetu halisi ya maji ni lita
milioni 214.6 ambapo uzalishaji katika kipindi hiki umefikia lita milioni 163
sawa na asilimia 76 ya mahitaji. Kutokana na takwimu hizi upatikanaji wa maji
katika Mkoa wa Mjini Magharibi umefikia asilimia 87.7, Mkoa wa Kusini Unguja
asilimia 76.45, Mkoa wa Kaskazini Unguja asilimia 71.68, Mkoa wa Kusini Pemba
asilimia 74.08 na Mkoa wa Kaskazini Pemba asilimia 56.42 ya mahitaji halisi.
ARDHI NA
MAKAAZI:
Mheshimiwa
Spika,
Serikali
iliahidi kushughulikia suala la matumizi bora ya ardhi kwa kuzingatia udogo wa
ardhi tuliyonayo. Katika utekelezaji wa azma hii, Serikali imetayarisha sera
mpya ya ardhi ili kusimamia na kutekeleza mipango ya matumizi bora ya ardhi.
Sera hiyo pamoja na mambo mengine imezingatia mabadiliko ya maendeleo ya
kijamii na kiuchumi yaliyopo na yatakayokuja baadae.
Kazi
ya usajili wa ardhi imeshafanywa katika zaidi ya shehia 20 na zoezi la utambuzi
linaendelea katika shehia 13. Jumla ya nyumba, viwanja na mashamba 22,398
vimeshatambuliwa sambamba na hatua hiyo, zoezi la utoaji wa Hati za matumizi ya
Ardhi linaendelea kwa kutoa hati mpya na kuzibadilisha zile za zamani. Hadi
sasa jumla ya mikataba ya matumizi ya ardhi 223 imeshasainiwa na kukabidhiwa
wawekezaji. Vile vile, hati 1,310 za matumizi mbali mbali ya ardhi zimetolewa
na viwanja 1,691 vimepimwa, Unguja na Pemba.
Mheshimiwa
Spika,
Katika
kukabiliana na tatizo la matumizi mabaya ya ardhi, Serikali imeshakamilisha
mpango mkuu wa matumizi ya Ardhi ya Mji wa Zanzibar na Mpango Mkakati wa
Maendeleo ya Ardhi Zanzibar, sambamba na mipango ya matumizi ya ardhi ya Mikoa
yote ya Zanzibar. Katika kuhakikisha uhifadhi wa Mji Mkongwe wa Zanzibar,
Serikali imeanzisha mfumo mpya kwa njia ya kuishirikisha Sekta ya Umma na Sekta
Binafsi (PPP) kwa ajili ya kuhifadhi nyumba ziliopo Mji Mkongwe. Mfumo huo
utafanywa kupitia Kampuni itakayoitwa Hifadhi Zanzibar na tayari imeshasajiliwa
na kuanza kazi zake. Aidha, Serikali inaendelea na matayarisho ya kuanzisha
Mfuko wa Maendeleo ya Miji ili kusimamia ustawi wa maendeleo ya miji yetu.
Nina
matumaini makubwa kuwa kupitia mipango hiyo, wananchi wataelimika na watazidi
kuifahamu mipango ya matumizi bora ya ardhi na utaratibu huu utapunguza
changamoto zilizopo hivi sasa. Nawasihi sana wananchi waendelee kushirikiana na
Serikali
katika utekelezaji wa mipango hii ili tuweze kufikia azma yetu ya matumizi bora
ya ardhi.
HABARI NA
MAWASILIANO:
Mheshimiwa
Spika,
Kwa
upande wa habari, katika kipindi cha miaka mitano, Serikali imeimarisha utoaji
wa habari kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kurusha moja kwa moja matangazo
yanayohusu vikao vya Baraza la Wawakilishi. Tumeliwezesha Shirika la Utangazaji
la Zanzibar (ZBC) kufanya mageuzi ya kutoka mfumo wa "Analogue"
kwenda "Digital" kwa mafanikio na kwa wakati tuliopangiwa na Jumuiya
za Kimataifa. Tumeongeza muda wa kutangaza, ambapo hivi sasa ZBC Radio na TV
zinakuwa hewani kwa saa 24. Vile vile, gazeti la Zanzibar Leo linalotolewa na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ubora wake wa habari na uchapishaji
umeongezeka na hivi sasa linapatikana kila siku katika maeneo mbali mbali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, Zanzibar imepiga hatua kubwa kwa
kuongeza idadi ya vyombo vya habari zikiwemo radio jamii 4 pamoja na vituo vya
habari binafsi. Hali hii imechangia sana kuongezeka kwa uhuru wa kupata habari
na kusukuma maendeleo ya jamii yetu katika nyanja mbali mbali.
Vile
vile, Serikali imetekeleza azma yake ya kuwajengea wasanii wetu “Studio” za
kisasa za kurekodia nyimbo na michezo ya kuigiza kwenye jengo la zamani la
Utangazaji la Sauti ya Tanzania Zanzibar, baada ya kufanyiwa matengenezo
makubwa.
Mheshimiwa
Spika,
Kwa
lengo la kutekeleza azma ya Serikali ya kukifufua Kiwanda cha Upigaji Chapa na
Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali ili kurudisha hadhi yake na kuinua
kiwango cha uzalishaji, jumla ya TZS milioni 5,532.40 zimetumika kwa
matengenezo ya majengo yaliyokuwa kiwanda cha sigara Maruhubi pamoja na ununuzi
wa mashine mpya za kisasa za uchapishaji za kiwanda hicho. Serikali ina lengo
la kukiimarisha zaidi ili kiweze kuchapisha magazeti, vitabu vikubwa na
kadhalika. Fedha kwa ajili ya kazi hio tayari zimepatikana kutokana na msaada
wa Serikali ya Oman. Ni dhahiri kukamilika kwa
kiwanda
hiki kumeipunguzia mzigo Serikali na kitaiwezesha kutoa huduma zenye ubora wa
kiwango kikubwa zaidi.
Mheshimiwa
Spika,
Kwa
lengo la kuziimarisha huduma za mawasiliano Serikalini, katika kipindi hiki cha
kwanza cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba, Serikali
imeanzisha mradi wa “e-government” ambao uliuzinduliwa mwezi wa Januari mwaka
2013. Hadi hivi sasa, jumla ya majengo 86 ya Serikali yameunganishwa katika
mtandao wa Serikali (e-government) na tayari yameanza kupata huduma ya
“internet” bila ya malipo.
Awamu
ya kwanza ya mradi huu inaendelea vizuri na maandalizi ya awamu ya pili
yamekamilika, ambapo huduma za “e-health” na nyengine zitaanzishwa. Hivi sasa
Serikali imo katika maandalizi ya kuiunganisha Zanzibar na Tanzania Bara
kupitia mkonga wa Taifa na ule wa kimataifa (ESSY).
UTAMADUNI NA
MICHEZO:
Mheshimiwa
Spika,
Kwa
lengo la kudumisha na kutangaza utamaduni wetu, silka na desturi zetu, Serikali
imefanikiwa kuandaa matamasha mbali mbali ambayo yamesaidia sana katika
kuendeleza na kuhifadhi utamaduni wa mambo ya asili. Kadhalika, kwa
kushirikiana na wana michezo, Serikali imefanikiwa na juhudi zake za kufufua na
kuimarisha michezo nchini. Ni jambo la kufurahisha kuona kuwa baadhi ya
wawakilishi katika Baraza la Wawakilishi wamekuwa mstari wa mbele katika jambo
hili kwa kuanzisha timu na vikundi vya michezo na mazoezi katika majimbo yao na
kuzipatia timu hizo vifaa mbali mbali.
Serikali
imeanzisha mashindano ya riadha ya Wilaya, kwa Wilaya zote kumi za Zanzibar na
timu za michezo mbali mbali, zimepatiwa vifaa. Viwanja vyetu vimeimarishwa na
hivi karibuni Serikali kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China
imeanza kukijenga upya Kiwanja cha Mao- Tze Tung.
Ni
jambo la kujivunia kuona kuwa, katika kipindi hiki cha kwanza cha Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba, yenye Muundo wa Umoja wa Kitaifa tumeweza
kuvijenga
upya Viwanja viwili vikubwa na vya kisasa; Kiwanja cha Kariakoo kwa Unguja na
Kiwanja cha Tibirinzi kwa upande wa Pemba. Kiwanja cha Kariakoo nilikifungua
rasmi tarehe 8 Januari, katika shamra shamra za Miaka 51 ya Mapinduzi. Vile
vile, Kiwanja cha Tibirinzi nacho tunaweza kukifungua wakati wowote kuanzia
Mwezi ujao. Viwanja hivi vitawapa watoto wetu sehemu nzuri ya kwenda kucheza na
kufurahia na kuwafanya wakue wakiwa na afya bora.
Mheshimiwa
Spika,
Ujenzi
wa Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ulioko Michenzani umo katika
hatua za mwisho za kumalizika. Niliweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mnara huu
tarehe 11 Januari, 2014. Ni dhahiri kuwa kumalizika kwa Mnara huu kutaongeza
idadi ya maeneo ya kutembelea na kupumzikia kwa wananchi wa Zanzibar na wageni
wanaotutembelea na watapata fursa ya kujifunza historia ya Mapinduzi yetu.
MAKUNDI MAALUM:
Mheshimiwa
Spika,
Mashirikiano
na mshikamano tuliouonesha katika kipindi hiki cha miaka mitano katika Serikali
yetu tumeweza kuinua hali na ustawi wa wanawake, vijana na watoto, na wazee
katika sehemu zote za Unguja na Pemba. Serikali imeweza kuwahudumia na
kuwatunza wazee kwa kuyaimarisha makaazi yao na kuwapatia huduma muhimu za kila
siku kwa maisha yao, kwa kiwango cha kuridhisha. Sheria Namba. 6 ya Mwaka 2011
mlioyoipitisha imetupa mwongozo imara katika kuweka mazingira bora ya
kupatikana haki muhimu za watoto wanaishi na kukua katika mazingira mbali
mbali. Mahakama ya watoto tuliyoifungua rasmi mwezi Februari mwaka 2013
inaendelea kuimarisha utoaji wa haki na kuongeza kasi katika uendeshaji wa kesi
zinazohusu masuala ya watoto. Pamoja na hatua hiyo, Serikali imefungua vituo
vya kushughulikia waathirika wa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia katika Hospitali
zetu za Mnazi Mmoja, Kivunge, Makunduchi na Chake chake vikiwa na wataalamu
wote wanaohusika katika kuchukua hatua.
Mheshimiwa
Spika,
Katika
kuifanikisha Kampeni ya udhalilishaji wa wanawake na watoto tuliyoizindua rasmi
tarehe 6 Disemba, 2014. Mwamko uliopo katika majimbo yenu umekuwa ni chachu ya
mafanikio makubwa tunayoyashuhudia katika Kampeni hii.
Katika
juhudi zinazoendelea kuchukuliwa za kuimarisha maslahi ya wazee. Serikali
imeamua kuanzisha malipo ya pencheni kwa wazee wote (Universal Pension). Kwa
kuanzia malipo haya yatatolewa kwa wazee wenye umri wa miaka sabiini (70).
Tathmini ya awali imebainisha kuwa jumla ya wazee 27,366 watafaidika na mpango
huu kwa kulipwa kila mwezi. Serikali tayari imeweka TZS bilioni 1.65 kwa ajili
ya malipo hayo kwa muda wa miezi mitatu ya mwanzo. Zoezi hili linatarajiwa
kuanza rasmi Aprili Mosi mwezi, 2016. Katika mpango huu, wazee wote wa Zanzibar
waliofikia umri huu watafaidika kwa kupewa TZS 20,000 kila mwezi bila ya kujali
historia ya kazi walizokuwa wakifanya kabla ya kufika umri huo. Imani yangu ni
kuwa utaratibu huu mpya tuliounzisha utasaidia wazee wengi walikuwa katika
ajira zisizo za Kiserikali, hasa wakulima na wajasiriamali, ambao walikuwa
wakijikuta hawana msaada wowote wakati wanapostaafu.
Vile
vile, katika kipindi hiki cha miaka mitano, Serikali imefanya jitihada mbali
mbali ili kuwasaidia watu wenye ulemavu. Mfuko Maalum wa Watu Wenye Ulemavu
umeanzishwa na niliuzindua mwaka 2012. Mfuko huu hivi sasa una jumla ya TZS
milioni 167.6 ambazo zitatumika kwa mahitaji mbali mbali ya watu wenye ulemavu.
Vile vile, Usajili wa watu wenye ulemavu uliofanywa kwenye Wilaya zote za
Unguja na Pemba sasa umekamilika, na umesaidia sana kuwatambua ili kurahisisha
upangaji na utekelezaji wa mipango yetu ya maendeleo. Kadhalika, Serikali
inaendelea kutoa ruzuku kwa Jumuiya za Watu wenye Ulemavu Unguja na Pemba ili
ziweze kutimiza malengo yao.
DEMOKRASIA NA
UTAWALA BORA:
Mheshimiwa
Spika,
Katika
hotuba yangu ya uzinduzi wa Baraza hili la Nane niliahidi kuwa Serikali
nitakayoiongoza itazingatia utawala bora wenye kuheshimu sheria na haki za
binaadamu. Vile vile, nilieleza kwamba nitaongoza nchi kwa misingi ya Katiba na
Sheria za Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nimefarajika kwa namna
ambayo tumeweza kutekeleza dhamira hizo. Katika kipindi hiki cha kwanza cha
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba, tumeweza kutekeleza mipango
mbali mbali kwa ajili ya kuimarisha Utawala Bora ikiwemo kuendelea kuunda
Wizara ya Nchi inayosimamia masuala ya Utawala Bora.
Juhudi
kubwa zilielekezwa katika kuhakikisha kuwepo kwa taasisi zilizo huru
zinazoendeshwa kwa kuzingatia Katiba na Sheria zinatekeleza majukumu yake kwa
uadilifu na mashirikiano. Serikali imeunda Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu
Uchumi baada ya Baraza hili kutunga Sheria Namba 1 ya mwaka 2012. Vile vile,
imeimarisha Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na
kuiwezesha kujenga na kuifungua Ofisi mpya Pemba kwa ajili ya kutekeleza
majukumu yake vizuri. Juhudi kubwa zimefanywa kuimarisha Ofisi ya Mkurugenzi wa
Mashtaka ikiwa ni pamoja na kuiongezea idadi ya wanasheria ili itekeleze
majukumu yake kwa ufanisi. Tume ya kupitia Sheria imeendelea na itaendelea na kazi
zake za kushauri kuondosha zile zilizopitwa na wakati na kuzifanyia marekebisho
zenye kuhitajika.
Kukamilika
kwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kufuatia mswada wa Sheria hiyo
uliopitishwa, tarehe 30 Januari, 2015, na Baraza hili ni hatua muhimu katika
kuimarisha Utawala Bora na demokrasia nchini. Nina imani kwamba viongozi wote
watatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria hii katika utendaji haki na
utoaji wa huduma zilizo bora kwa wananchi.
Mheshimiwa
Spika,
Serikali
inaendelea kutekeleza mageuzi kwenye mfumo wa kiutawala kwa kuzipa uwezo zaidi
Serikali za Mitaa ikiwa ni hatua muhimu ya kuimarisha Utawala Bora. Serikali
imeandaa Sera ya Serikali za Mitaa pamoja na Mpango wa Utekelezaji. Natoa
shukurani kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa michango mbali mbali
iliyowezesha kuifanyia marekebisho Sheria Namba 3 na 4 ya mwaka 1995 na Sheria
Namba 1 ya mwaka 1998 hadi ikatungwa Sheria mpya ya Tawala za Mikoa na Sheria
mpya ya Serikali za Mitaa za mwaka 2014. Aidha, natoa shukurani kwa wananchi
kwa kutuunga mkono katika utekelezaji wa mageuzi haya.
Ni
dhahiri kuwa mafunzo yaliyotolewa kupitia Semina Maalum kwa viongozi wa ngazi
mbali mbali yalikuwa ni chachu ya kuwapa maarifa mapya na kuongeza uzoefu wenu
na hatimae yaliwezesha kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi zadi. Utaratibu
tulioanzisha wa kuziita Ikulu Wizara zote za Serikali kuja kuwasilishaTararifa
za Utelezaji wa Mpango Kazi kila baada ya robo mwaka umetuwezesha kutekeleza
majukumu yetu kwa uwazi na kuimarisha uwajibikaji, mashirikiano na mahusiano
baina ya Idara mbali mbali za Wizara za Serikali.
Kadhalika,
utaratibu huu umetusaidia kupunguza muingiliano wa majukumu baina ya Wizara
moja na Wizara nyengine. Aidha, mpango huu umepanua upeo na maarifa katika
kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo kwa mujibu wa vipaumbele na
upatikanaji wa rasilimali fedha na watu. Haya yote ni mafanikio tuliyoyapata
katika kuleta uwazi na uwajibikaji ambayo ni mambo ya msingi katika Mfumo wa
Serikali ninayoiongoza.
Mheshimiwa
Spika,
Katika
kipindi cha miaka mitano, Serikali imechukua hatua mbali mbali za kuimarisha
Manispaa ya Zanzibar pamoja na miji ya Chake Chake, Wete na Mkoani, Serikali
ilianzisha Mradi wa Huduma za Jamii (ZUSP) mwaka 2011. ili kuimarisha upatikanaji
wa huduma muhimu katika miji hiyo, kuimarisha haiba, mazingira pamoja na
kuhifadhi eneo la urithi wa Mji Mkongwe.
SEKTA YA SHERIA:
Mheshimiwa
Spika,
Katika
kipindi cha miaka mitano hii, Serikali imechukua hatua kadhaa za kuimarisha
mazingira ya utendaji kazi katika Mahkama kwa lengo la kuongeza ufanisi katika
kazi zake, kupunguza mrundikano wa kesi na kuimarisha maslahi ya wafanyakazi.
Serikali imeyafanyia matengenezo makubwa majengo ya mahkama likiwemo jengo la
kihistoria la Mahkama Kuu Vuga na Mahkama nyengine nchini.
Kwa
upande wa majaji, Serikali imefanikiwa kuongeza idadi yao kutoka wawili mwaka
2011 hadi sita (wakiwemo wanawake wawili) mwaka 2014, sawa na ongezeko la
asilimia 200. Kwa upande wa Mahakimu wa ngazi mbali mbali, Serikali imefanikwa
kuongeza idadi yao kutoka 43 mwaka 2010 hadi 85 mwaka 2015. Hii ni sawa na
ongezeko la asilimia 97.7. Kadhalika, Serikali imeiongeza bajeti ya Mahakama
kutoka TZS bilioni 1.3 mwaka 2010/2011 hadi TZS bilioni 5 mwaka 2013/2014. Hii
ni sawa na ongezeko la asilimia 284.6.
Mheshimiwa
Spika,
Wakati
huo huo, katika kipindi cha miaka mitano, Afisi ya Mufti wa Zanzibar imeendelea
kuratibu na kusimamia majukumu yake ya kisheria. Katika kipindi cha miaka
mitano, watendaji wa Afisi ya Mufti wametembelea Madrasa za Kurani 164 na
Misikiti 166 na kutoa ushauri juu ya maendeleo ya taasisi hizo. Aidha, Madrasa
500 za taasisi za kidini 73 zimepatiwa usajili pamoja na kurushwa hewani kwa
vipindi 124 vya nasaha na mawaidha ya mafundisho ya kiislamu kupitia Radio ya
ZBC. Vile vile, Afisi ya Mufti imeshughulikia na kutatua migogoro mbali mbali
pamoja na kuhamasisha amani na utulivu.
Kadhalika,
Serikali imefanya jitihada mbali mbali katika kipindi hiki cha miaka mitano ya
kuziimarisha Mahakama za Kadhi ili kuendesha shughuli zake kwa ufanisi na
haraka. Jitihada hizo ni pamoja na kuongeza idadi ya makadhi kutoka 12 hadi 15
na kuimarisha mazingira ya kufanyia kazi kwa kuyafanyia matengenezo makubwa
majengo ya Ofisi za
Mahakama
na kuzipatia vifaa na samani. Hatua hizo zimechangia sana katika kuongeza
ufanisi na kupunguza malalamiko ya wananchi kuchelewa kufanyiwa kazi mashauri
yao.
Mheshimiwa
Spika,
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, imefanya jitihada kubwa ya kuiimarisha Mahakama ya
Ardhi ili kuiongezea uwezo wa kutatua migogoro ya ardhi. Idadi ya Mahakimu
katika Mahakama hiyo imeongezwa kutoka Mahakimu wawili hadi wanane katika
kipindi hiki cha awamu ya saba. Hatua hiyo imeiwezesha Mahakama kupunguza
mrundikano wa kesi za migogoro ya ardhi kutoka 800 hadi 200. Mazingira ya
kufanyia kazi yameimarishwa ambapo Mahakama hiyo inatumia jengo lilioko mjini
na Koani Unguja na kwa upande wa Pemba ipo Mahakama ya Wete na Chake Chake.
Hivi sasa mashauri ya migogoro ya ardhi yanafanyika kwa haraka zaidi
ikilinganishwa na miaka iliyopita jambo ambalo limepunguza kwa kiasi kikubwa
malalamiko ya wananchi.
Katika
kipindi hiki cha miaka mitano, Serikali imefanya jitihada za makusudi za
kuimarisha Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka kwa lengo la kuongeza uwajibikaji na
umahiri wa kisheria katika usimamizi wa mashtaka. Idadi ya Wanasheria wa
Serikali imeongezwa kutoka 28 waliokuwepo mwaka 2010 hadi kufikia 50 mwaka
2015. Ongezeko hili ni sawa na asilimia 78.5. Ongezeko hilo limeiwezesha Ofisi
ya DPP kuendeleza mashtaka ya kiraia (kuwatumia Wanasheria badala ya polisi)
katika mahkama za Mikoa yote na Wilaya sita. Wilaya nne zilizobakia
zinatarajiwa kuwa na utaratibu huu katika utekelezaji wa mipango iliyobainishwa
katia bajeti mliyoipitisha hivi karibuni ya 2015/2016. Nina imani kuwa hatua
hiyo iliyofikiwa itazidisha imani ya wananchi kwa Mahakama zetu na hukumu
zinazotolewa.
BARAZA LA
WAWAKILISHI:
Mheshimiwa
Spika,
Natoa
shukurani kwa mara nyengine kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Nane kwa
kuendelea kuweka misingi bora ya utawala bora na demokrasia. Kwa hakika mmeweza
kutekeleza vyema wajibu wenu wa kikatiba wa kutunga sheria na kuisimamia
Serikali
kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 5A(1) na kufafanuliwa kifungu 5A(2) cha
Katiba ya Zanzibar ya 1984.
Katika
kipindi cha miaka mitano, mmefanya majukumu yenu kwa kufanya mikutano yenu
katika hali ya salama na utulivu. Licha ya kutofautiana kwa hoja na mitazamo
kwa baadhi ya masuala muhimu, mmeweza kupitisha miswada ya sheria 63 na baadae
iliwasilishwa kwa Rais kwa ajili ya kutia saini na sasa zimekuwa sheria kamili.
Takwimu
zinaonesha kuwa katika kipindi hiki cha miaka mitano, maswali 1558 ya msingi na
maswala ya nyongeza (3103) yameulizwa kwa Serikali na yalipatiwa majibu sahihi.
Kamati teule 5 mlizoziunda nazo zimetekeleza majukumu yake kwa uadilifu na
umakini mkubwa. Nawapongeza wajumbe wote wa kamati teule hizo kwa kufuatilia na
kuibua masuala juu mambo mbali na kuyaleta Barazani kwa kujadiliwa na baadae
kuishauri Serikali juu ya mambo yanayoibuka. Aidha, nalipongeza Baraza kwa
kupokea na kujadili hoja binafsi zinazowasilishwa.
Baraza
hili la Nane limeingia katika historia ya nchi yetu, na litakumbukwa kwa
kipindi kirefu kijacho katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushiriki
katika Bunge Maalum la Katiba kwa lengo la kuunda Katiba Inayopendekezwa ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Napenda nikushukuruni nyote Waheshimiwa
Wajumbe kwa ushiriki wenu huo uliotuwezesha kupata Katiba Inayopendekezwa
ambayo hivi sasa wananchi wanaisubiri kwa hamu kuipigia kura ya maoni.
Leo
ni siku ya furaha kwa upande mmoja na siku ya huzuni kwa upande mwengine.
Nasema hivi kwasababu tunalivunja Baraza hili kwa mbwembwe na madaha kutokana
na mafanikio makubwa tuliyoyapata katika kuiendeleza nchi yetu. Leo ni siku ya
huzuni kwa sababu tunaagana na nitalivunja rasmi Baraza hili la Nane na huenda
ikapita kipindi bila ya baadhi yetu kuonana ingawa tunategemeana kwa kiasi
kikubwa.
Mheshimiwa
Spika,
Kwa
wale wenye dhamira ya kurejea majimboni kwa ajili ya kutafuta ridhaa ya
wananchi kwa mara nyengine, nawatakia mafanikio ili warudi tena kwa miaka
mitano myengine.
Kwa
wale ambao wamefikia uamuzi ya kutogombea tena, nawasihi waendelee kutumia
maarifa na uzoefu walioupata katika baraza hili katika kuongoza, kuhamasisha na
kushiriki kikamilifu katika harakati za maendeleo ya nchi yetu. Nyote mtabaki
kuwa hazina kubwa katika kupanga na kutekeleza mipango ya nchi hii.
Hata
hivyo, kwa wale mtakaojaaliwa kuchaguliwa tena na wananchi na kurudi Barazani,
nataka nikunasihini na nikukumbusheni kuwa mnapokuwa kwenye Baraza hili
muendelee kuizingatia, kuitii na kuitekeleza kwa vitendo Katiba ya Zanzibar,
sheria ziliopo na kanuni za Baraza hili. Baraza la Wawakilishi ni muhimili
uliowekwa ndani ya Katiba. Hiki ni chombo kikubwa kinachoendeshwa kwa misingi
ya Utawala Bora. Hakiendeshwi kwa kuendesha migomo au njia nyengine yoyote ya
ubabe. Baraza ni chombo cha wananchi wa Zanzibar kwa hivyo, suala lolote lenye
maslahi ya wananchi, hapa ndipo pahala pa kisheria pakulizungumza jambo hilo.
Kutoka
nje ya Baraza si ufumbuzi wa tatizo linalohusu hoja inayojadiliwa Barazani au
hoja nyengine iliyokuwa haijadiliwi na Baraza. Waheshimiwa Wajumbe nyinyi ndio
mnaotunga sheria za nchi, kwa hivyo nakunasihini msichanganye mambo. Kila
sheria iliyotungwa na Baraza hili matumizi yake yako wazi kwa kupitia taasisi
iliyowekwa. Nyinyi ni Waheshimiwa na wananchi na jamii kwa jumla
wanakuheshimuni na vile vile wanaliheshimu Baraza letu. Ni matarajio yangu
kwamba nanyi Waheshimiwa mtairejesha heshima hiyo kwao kwa kuwatimizia
matarajio yao ili tupate maendeleo zaidi.
Mheshimiwa
Spika,
Kila
mmoja wetu anaelewa kwamba Baraza lako linaendeshwa kwa misingi ya Sheria na
Kanuni. Hoja zinazotolewa na kujadiliwa na baraza hili zinaendeshwa kwa misingi
hiyo. Wakati Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa chama cha CUF waliposusia
kikao cha tarehe 23 Juni, 2015, hoja walizozitoa hazikuwa na mnasaba na hoja
iliyokuwa imewasilishwa barazani ili ijadiliwe kwa wakati huo. Siku hiyo Waziri
wa Fedha alikuwa amewasilisha hoja ya kujadiliwa kwa Mswada wa Sheria ya
Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ambao haukuwa na uhusiano
hata kidogo na masuala ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga
kura. Hoja yao inahusiana na Sheria nyengine, Sheria ya Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar, Nam. 9 ya mwaka 1992 inayosimamiwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar
pamoja na Sheria ya Usajili wa Mzanzibari Mkaazi, Nam. 7 ya mwaka 2005.
Mheshimiwa
Spika,
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuhakikisha kila mwananchi mwenye sifa ya
kupiga kura anapewa haki yake. Wanasiasa wasipotoshe wananchi juu ya haki hiyo.
Nawanasihi viongozi wote wa siasa waiache Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ifanye
kazi yake ikiwa huru na isiingiliwe kwa namna yoyote ile. Ni wajibu wetu sote
kuheshimu sheria na kushirikiana na Tume ili kuhakikisha tunakuwa na Uchaguzi
ulio Huru na Haki.
Kuanzia
sasa macho ya ulimwengu yanatuangalia. Nasema tusonge mbele kwa heshima na nia
safi ya kuendeleza mafanikio yetu kama nilivyoyaeleza muda mfupi uliopita.
MASUALA
MENGINEYO:
AMANI NA
USALAMA:
Mheshimiwa
Spika,
Siri
kubwa ya mafanikio yetu katika sekta zote za maendeleo nilizozielezea ni
kuendelea kuimarika kwa hali ya amani na utulivu nchini. Kwa nyakati mbali
mbali nimekuwa nikisisitiza umuhimu wa kusimamia amani na utulivu wa nchi yetu
kwa vile ni rasilimali
ya
msingi ambayo kila mwananchi anapaswa kuilinda kuiendeleza na kuienzi kwa nguvu
zake zote.
Katika
hotuba yangu ya uzinduzi wa Baraza hili la Nane la Wawakilishi nilisema,
napenda ninukuu:
“Suala
la kudumisha amani si la Idara Maalum Na Vikosi vyetu vya Ulinzi Na Usalama
peke yake, lakini linashirikisha wananchi wote kwa jumla”
Nimefarajika
na mafanikio makubwa tuliyoyafikia katika kutekeleza wajibu wetu huo kwa
vitendo. Katika kipindi chote cha miaka mitano, Idara maalum za SMZ, Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
vimetekeleza vyema jukumu lao la kusimamia ulinzi, amani na utulivu kwa
kuhakikisha maisha ya watu na mali zao yamekuwa salama. Napenda nitumie fursa
hii kuwapongeza sana kwa utekelezaji mzuri wa dhamana zao hizo.
Mheshimiwa
Spika,
Hali
ya amani na utulivu nchini imechangiwa sana na wananchi walio wengi kutambua
kuwa vitendo vinavyosababisha kuvunjika kwa amani vina athari kubwa kwa maisha,
uchumi na maendeleo ya ustawi wa jamii yetu. Naamini kuwa wachache waliojaribu
kuichezea amani kwa visingizio mbali mbali hawakuwa wakifurahiwa na wananchi
wengine ila ni kwa sababu ya kukidhi malengo yao binafsi.
Napenda
nisisitize kwamba kila mmoja wetu atilie maanani kuwa utii wa sheria ni hatua
muhimu katika kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa na amani, utulivu na kupata
maendeleo zaidi. Kwa hivyo, ni jukumu la viongozi wote wa Serikali, wanasiasa,
viongozi wa madhehebu ya dini, viongozi wengine katika jamii na wananchi wote
kwa jumla kutekeleza wajibu wetu wa kuhakikisha tunadumisha amani na utulivu na
sheria zinafuatwa. Kutii Katiba ya Zanzibar na sheria zake si jambo la hiari
bali ni wajibu wetu sote na msingi muhimu wa kulinda amani na utulivu wetu.
Nataka nikuhakikishieni, Waheshimiwa Wajumbe na niwahakikishie wananchi wote wa
Zanzibar kwamba
nitaendelea
kuisimamia amani na utulivu kwa nguvu zangu zote. Nitamchukulia hatua yeyote
atakayejaribu kuivunja amani ya Zanzibar.
MUUNGANO:
Mheshimiwa
Spika,
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba inatambua na inazingatia haja ya
kuimarisha muungano wa Tanzania kama nguzo ya pili muhimu baada ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 kwa malengo yale yale ya waasisi wetu,
Marehemu Mzee Abeid Amani Karume na Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Ni dhahiri kuwa nguzo zetu hizi; Mapinduzi na Muungano ndizo zimetuwezesha
kupiga hatua kubwa za maendeleo yetu kisiasa, kiuchumi na kijamii na kuleta
heshima ya Wazanzibari na watanzania mbele ya mataifa mbali mbali katika
kipindi cha miaka 51.
Katika
kipindi hiki cha miaka mitano, Muungano wetu umezidi kuimarika kutokana na
hatua zinazochukuliwa na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hatua hizo ni pamoja na kuzifanyia
kazi zile zinazotambuliwa kuwa ni kero za muungano. Masuala kadhaa
yameshatatuliwa kupitia Kamati inayoongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inawajumuisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Aidha, vikao vya kuimarisha
mashirikiano ya kisekta kati ya Wizara za Serikali ya Muungano wa Tanzania
vimeendelea kufanywa na kuratibiwa kupitia Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
Mheshimiwa
Spika,
Miongoni
mwa mafanikio ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya Saba, ni mchango
wa Serikali katika mchakato wa kupata Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ulioasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk.
Jakaya Mrisho Kikwete kwa lengo la kuimarisha muungano wetu. Kwa mara nyengine,
napenda nimpongeze Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuanzisha
mchakato
wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kushirikiana katika
hatua zote na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Sote
tunatambua na tunathamini kazi nzuri iliyofanywa na Waheshimiwa Wabunge wa
Bunge la Katika la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutupatia Katiba
inayopendekezwa tuliyokabidhiwa mimi na Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete tarehe
08 Oktoba, 2014 katika Uwanja wa Jamhuri pale Dodoma. Kazi iliyo mbele yetu
wananchi wote ni kushiriki katika Kura ya Maoni wakati utakapofika ili tuweze
kunufaika na mambo mengi ya msingi yaliyozingatiwa katika kuandaa Katiba
inayopendekezwa.
USHIRIKIANO
NA NCHI NYENGINE NA WAZANZIBARI WANAOISHI NJE:
Mheshimiwa
Spika,
Zanzibar
ikiwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; imeendelea kushirikiana na
nchi nyengine. Vile vile kitengo maalum kinachoratibu masuala ya Wazanzibari
wanaoishi nchi za nje, kimeanzishwa kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Maofisa wetu katika kipindi hiki wameshiriki katika
mikutano mbali mbali ya kikanda. Wazanzibari wanaoishi nchi za nje wamekua wakitoa
michango mbali mbali ya fedha na kitaalamu hasa katika sekta ya elimu, afya,
utalii, biashara na uwekezaji. Vile vile, Ofisi ya Rais Ikulu imeandaa
utaratibu wa kukutana na Wana “Diaspora” kila mwaka kwa kualikwa Ikulu
kubadilishana mawazo pamoja na Rais.
Uhusiano
wetu umezidi kuimarika kwa kupata fursa ya kutembelewa na viongozi wa nchi
kadhaa, taasisi za kimataifa, mabalozi na kufanya ziara katika nchi mbali mbali
mimi na viongozi wenzangu wakuu wa Serikali. Kadhalika, kipindi hiki, cha miaka
mitano nilipata fursa ya kufanya ziara za kuzitembelea nchi kadhaa kwa lengo la
kuuimarisha uhusiano wetu.
Kadhalika,
kwa nyakati tofauti nilikutana na Mabalozi, Wawakilishi wa taasisi mbali mbali
za Kimataifa na viongozi wa nchi mbali mbali ambao walikuja kuonana nami na
kufanya mazungumzo.
Katika
mazungumzo yetu na viongozi hao tuliweza kuimarisha uhusiano wetu katika nyanja
mbali mbali za maendeleo zikiwemo za kiuchumi na biashara, mazingira, elimu, na
uimarishaji wa sekta ya afya na utamaduni na sekta ya utalii. Faida ya
makubaliano yetu zimeanza kupatikana katika utekelezaji wa mipango na miradi
mbali mbali nchini.
MWISHO:
Baada
ya maelezo yangu ya kina ya utendaji na mafanikio ya Serikali ninayoiongoza
tangu tarehe 3 Novemba, 2010 ambayo imetekeleza asilimia 90 ya Ilani ya Chama
tawala, Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2010 – 2015, napenda kutoka shukurani
zangu nyingi kwa Waheshimiwa Wajumbe kwa kunisikiliza kwa makini. Safari yetu
bado haijafika mwisho na najua tumo katika matayarisho ya kuanza sehemu ya pili
ya Awamu hii.
Nachukua
fursa hii kutoa shukurani kwenu nyote kwa muda mlioutumikia kuzifanikisha
shughuli za Baraza la Nane, kupitia vikao vya Baraza na Kamati zake mbali
mbali. Sote tumetimiza wajibu wetu na tutaendelea kuwatumikia wananchi kila
tutakapopata fursa ya kuwatumikia.
Mheshimiwa
Spika,
Natoa
shukurani za dhati kwa wasaidizi wangu wakuu, Makamu wa Kwanza wa Rais; Mhe.
Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais; Mhe. Balozi Seif Ali Iddi
kwa ushauri wao na kunisaidia katika kuzifanikisha kazi za Serikali katika
utekelezaji wa kazi zetu za kila siku. Kadhalika, shukurani zangu ziende kwa
Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri wote, Makatibu Wakuu na Manaibu wao,
Wakurugenzi, Watendaji na Watumishi wote wa Serikali kwa ushirikiano walionipa
na kwa kazi nzuri ya kuwatumikia wananchi. Kadhalika, natoa shukurani maalum
kwa Wajumbe na Watendaji wa Mabaraza ya Miji na Halmashauri za Wilaya zote na
Wananchi kwa jumla kwa ushirikiano walioipa Serikali katika utekelezaji wa
mipango mbali mbali ya maendeleo.
Nathamini
sana moyo wa uzalendo na kujituma waliouonesha wananchi pamoja na kuendeleza
hali ya amani na mshikamano. Jambo hili limepelekea kuwepo kwa
mashirikiano
mazuri kwa Serikali na Wananchi katika kushughulikia masuala muhimu ya
maendeleo. Vile vile, kwa muda wote Serikali yetu imepata sifa kubwa katika
kusimamia amani, utulivu na kuwaletea wananchi wake maendeleo. Sifa nyingi na
shukurani hizo ambazo hufikishwa kwangu na Viongozi, Mabalozi na Washirika wetu
wa Maendeleo ninaopata fursa ya kukutana nao ziwaendee wananchi wa Zanzibar.
Kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Wananchi wote napenda
Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza hili mzipokee shukurani hizo kwa mchango wenu
mkubwa na kwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kutuletea maendeleo. Ahsanteni
Sana.
Nawatakia
kheri wale Waheshimiwa ambao kwa sababu mbali mbali hawatakuwemo katika Baraza
lijalo baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015. Wale wanaowania kurejea
pamoja na wengine ambao sasa si Wajumbe nawasihi wazingatie utunzaji wa amani
na utulivu katika harakati zao za uchaguzi. Huu ni wakati wetu sote
kudhihirisha ustaarabu katika siasa zetu, umoja wetu, mshikamano na utiifu wa
sheria. Utunzaji wa amani ni dhamana yetu sote.
Kwa
mara nyengine tena nasisitiza kwamba Serikali zetu mbili na vyombo vyake vya
sheria, ulinzi na usalama havitomvumilia yeyote atakaehatarisha amani na
kufanya fujo. Natoa wito kwa vijana wasishawishike kufanya fujo kwa sababu
yoyote ile.
Mheshimiwa
Spika,
Kwa
mara nyengine tena natoa shukurani zangu za dhati kwako Mhe. Pandu Ameir
Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi kwa kuliongoza Baraza hili kwa busara,
haki, uadilifu na ufanisi mkubwa. Umefanya kazi kubwa ya kuliendesha Baraza
hili kwa uadilifu mkubwa. Umetoa mchango mkubwa katika kukuza demokrasia na
Utawala Bora. Nakutakia kila la kheri katika maisha yako.
Mheshimiwa
Spika,
Ili
kutoa nafasi kwa matayarisho ya mwisho kwa ajili ya uchaguzi mkuu ifikapo
tarehe 25 Oktoba 2015, kwa madaraka niliyo nayo kama ilivyoelezwa katika
kifungu cha 91 (2) (a) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984,
natamka kwamba kuanzia Alkhamis tarehe
13 Agosti 2015 Baraza la Nane la Wawakilishi la Zanzibar limevunjwa rasmi.
Nakutakieni kila la kheri na
Ramadhani njema
MUNGU IBARIKI ZANZIBAR
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRIKA
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
0 comments:
Post a Comment