MAKOCHA WAZUNGU WA SIMBA NI NOMA!!

13:29 by Kwetuhouse Media

Wachezaji wa Simba wakifanya mazoezi.

SIKU chache tangu Simba ilipotua Tanga kujiandaa na msimu mpya, wachezaji wa timu hiyo wamekiri kuwa mazoezi ya kocha wao mkuu, Dylan Kerr ni balaa kwa kuwa ni ya kiwango cha juu.

Simba ipo chini ya Kerr na msaidizi wake, Selemani Matola pamoja na kocha wa viungo, Mserbia, Dusan Momcilovic na kocha wa makipa, Mkenya, Abdul Idd Salim.Wakizungumza na Championi Ijumaa kwa nyakati tofauti, wachezaji wa timu hiyo walisema mazoezi wanayopata ni ya kiwango cha juu.

Nahodha mpya wa timu hiyo, Mussa Mgosi, alifunguka: “Hauwezi amini tangu tumefika Lushoto na kuweka kambi ya kujiandaa na ligi kuu, sijapata muda kabisa wa kuchati na simu kutoka kwa ndugu na marafiki zangu.

“Tunachoka sana kutokana na mazoezi ya nguvu, hivyo muda mwingi mimi binafsi ninautumia kulala na mazoezi peke yake.“Mazoezi ya kiwango cha juu, tunachoka sana na hata tukitoka mazoezini haukuti mtu yupo nje zaidi ya kuwakuta vyumbani wamelala.”

Kwa upande wa straika wa Simba, Elias Maguli, alisema: “Tunatumia muda mwingi baada ya mazoezi kulala kutokana na mazoezi ya nguvu.”Akizungumzia hali hiyo, Matola alisema: “Huyu kocha ni wa kiwango cha juu, mazoezi yake ni ya kiwango cha juu kwa kweli, nimefanya kazi na makocha wengi wa nje lakini huyu ni mmoja wa walio bora kabisa.”

0 comments:

Post a Comment