Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade),
Jacqueline Mneney Maleko (wa tatu kushoto) akiongozana na Mratibu Mkazi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili
katika viwanja vya maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba',
barabara ya Kilwa, jijini Dar.(Picha zote na Zainul Mzige wa
Modewjiblog).
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade),
Jacqueline Mneney Maleko (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na
Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakati wakielekea katika
banda la Shirika la Umoja wa Mataifa lilipo Karume Hall mara tu baada ya
kuwasili.
Na Modewjiblog team, Sabasaba
Mratibu
mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP)
nchini, Alvaro Rodriguez, akizungumza na waandishi wa habari
alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa leo katika maonyesho ya 39 ya
kimataifa ya biashara Sabasaba amesema Tanzania imekuwa mstari wa mbele
katika utekelezaji wa miradi na mikakati ya Umoja wa Mataifa miongoni
mwa nchi za Afrika Mashariki.
Ameongeza
kuwa dunia sasa imekuwa kijiji kimoja na Umoja wa Mataifa umekuwepo
Tanzania hata kabla ya uhuru, hivyo unakusudia kuendelea kuwepo
kushirikiana na watanzania katika kutatua matatizo kwenye Nyanja
mbalimbali.
Bw.
Alvaro amewataka watanzania kusherehekea pamoja miaka 78 ya Umoja hapa
nchini kwa kutoa maoni mbali mbali na kushiriki kikamilifu katika miradi
ya maendeleo.
Amesema
kwa pamoja tunahitaji kuzungumzia usawa wa kijinsia, masuala ya
kisiasa, mabadiliko ya tabia nchi na mambo ya kiuchumi kwa ajili ya
ustawi wa taifa.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan
Trade), Jacqueline Mneney Maleko, ameushukuru Umoja wa Mataifa kwa
kufanya juhudi za kusaidia vijana kuanzia ngazi za chini kabisa na
kuwawezesha kuwa wajasiriamali.
Amesema
kitendo cha Umoja huo kushiriki katika maonyesho ya Sabasaba sambamba
na kijana Amos Mtambala waliyemuwezesha kwa kumpatia mafunzo ya sanaa za
uchoraji kumeleta hamasa kubwa miongoni mwa vijana wasio na ajira
nchini.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez akisaini kitabu cha wageni
mara baada ya kuwasili kwenye banda la Shirika la Umoja wa Mataifa
katika viwanja vya maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba',
barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade),
Jacqueline Mneney Maleko akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la
Umoja wa Mataifa.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania,
Hoyce Temu, akitoa maelezo jinsi wanavyoelimisha wananchi kuhusiana
shughuli mbalimbali za Umoja wa Mataifa nchini sambamba na malengo ya
millenia yanayofikia kileleni kwa Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez aliyeambata na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko
walipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya 39 ya kimataifa ya
biashara 'Sabasaba', katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya
Kilwa, jijini Dar.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu akielezea maeneo ya Program mbalimbali za UNDAP yaliyofanikiwa
nchini Tanzania kwa Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
(kulia) aliyeambata na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu akikabidhi taarifa ya mwaka ya UNDAP kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko
(katikati) aliyefuatana na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
(kulia) walipotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa lililopo
Karume Hall.
Mkurugenzi
na Meneja mradi wa TUBEGA ART ambaye ni mtaalamu wa sanaa za uchoraji,
Amos Mtambala, akitoa maelezo jinsi alivyowezeshwa kupitia Shirika la
Kazi Duniani (ILO) kupata elimu inayomwezesha kuwa mjasiriamali kwa
kuuza michoro hiyo ndani ya banda la Umoja wa Mataifa kwa Mratibu Mkazi
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alipotembelea banda la Shirika la Umoja
wa Mataifa lililopo Karume Hall ndani ya viwanja vya maonyesho ya 39 ya
biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”.
Afisa
Mawasiliano wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) nchini, Magnus Minja
akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
kuhusiana na program ya kazi njenje ya mradi wa kufundisha vijana katika
shughuli za ujasiriamali inayoratibiwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO)
ambapo kijana Amos iliweze kumuinua na kujiajiri kupitia sanaa ya
uchoraji.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade),
Jacqueline Mneney Maleko, akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) moja ya karatasi inayotoa maelezo ya jinsi ya Watanzania
wanavyoweza kushiriki kutoa maoni mbalimbali juu ya utendaji wa Shirika
la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kutuma SMS ambayo ni bure bila
malipo yoyote na moja kwa moja kumfikia Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini
Alvaro Rodriguez.
Jinsi
ya kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), kwa kuandika neno UN au
UMOJA WA MATAIFA ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Airtel watatuma
ujumbe wao kwenda namba 15453, kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo
wanatuma kwenda 15055 au 15453 na kwa Vodacom ni namba 15055.
Ambapo pia njia nyingine ya kuwasilisha maoni ya moja kwa moja ni kupitia mtandao wa (Online) kwa kubofya link hii http://gpl.cc/UN2
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade),
Jacqueline Mneney Maleko akizungumza na waaandishi wa habari katika
banda la Shirika la Umoja wa Mataifa ambao wanashiriki maonyesho ya 39
ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba', katika viwanja vya Mwl. J.K
Nyerere, vilivyopo barabara ya Kilwa, jijini Dar. Kushoto ni Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline
Mneney Maleko mfuko wenye machapisho na vijarida mbalimbali vya Umoja wa
Mataifa.
Afisa
Utawala wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Suleiman Magoma
(wa pili kushoto) akiuliza swali kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro
Rodriguez (kushoto) wakati alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa
lililopo Karume Hall katika maonyesho ya Sabasaba. Kulia ni Afisa Habari
wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama na
Wa pili kulia ni Mchumi wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Vainess Molle.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez akijibu swali la Bw. Suleiman.
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma
Ledama akionyesha namna ya kutoa maoni ya utendaji wa Shirika la Umoja
wa Mataifa Tanzania kwa njia ya SMS ambayo ni bure kwa mitandao yote ya
simu za mkononi nchini kwa wadau waliotembela banda la UN Tanzania.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez ajibu maswali mbalimbali
yalitumwa kwa njia ya mtandao na wananchi katika banda la Umoja wa
Mataifa maonyesho ya Sabasaba.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko
katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaotoa
huduma katika banda la Umoja wa Mataifa maonyesho ya Sabasaba.
0 comments:
Post a Comment