Mradi wa nyumba unaosimamiwa na
kampuni ya Hifadhi inayoitwa Dege Eco-Village umeshiriki Maonyesho ya Biashara
ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam ya Saba Saba.
Akiongea na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa
Dege eco-Village alisema “Kwa sasa ujenzi unaendelea na karibu aina ya nyumba
apartment 3000 zishakamilika.
Aliongezea kusema kwamba kupitia
mradi huu waTanzania watanufaika kwa kupata ajira na pia kuwa na huduma kama
hospitali, shule, maduka eneo la Kigamboni.
Mradi huu unajengwa kwenye eneo
takriban eka 300 na kampuni hiyo imewekeza zaidi ya dola milioni 350. Kwa
ujumla nyumba aina ya villa ziko 300 na apartment ziko 7400. Mradi huu
utakamilika mwaka 2018. Apartment zitakamilika mwaka 2017 na villa mwaka 2018.
Ndani ya mji huu wa Dege
Eco-Village wa kazi hawatahitaji kwenda popote kwasababu kila kitu kitakuwepo
kama shule za watoto, kituo cha polisi, hospitali, supermarket, na kadhalika.
Wafanyakazi wa Dege Eco –
Village wakiwahudumia wateja wao waliofika katika banda lao.
Wafanyakazi wa Dege Eco –
Village akimhudumia wateja wao waliofika katika banda lao.
Wafanyakazi wa Dege Eco –
Village amkimpa maelekezo mteja aliyefika bandani kwao kuchangamkia fursa ya
kununua nyumba.
Mkurugenzi
wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege Eco-Village (katikati) akiwaonyesha
wafanyakazi wa kampuni hiyo namna walivyoweza kufanya vyema katika mauzo ya
nyumba.
Wafanyakazi wakiwa katika
picha ya pamoja.
0 comments:
Post a Comment