Waziri wa nchi ofisi ya rais (kazi maalumu) Prof Mark
Mwandosya(picha kutoka Maktaba)
Serikali imeuondoa
muswaada wa sheria ya haki ya kupata habari 2015 uliokuwa uwasilisilishwe na
kujadiliwa katika mkutano unaoendelea wa bunge mjini Dodoma ili kutoa nafasi
kwa wadau kutoa maoni yao.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (asiye na wizara maalum) Prof Mark Mwandosya ameliambia
bunge leo asubuhi kuwa serikali imefikia uamuzi huo kutokana na maoni ya kamati
ya kudumu ya bunge ya maendeleo ya jamiii iliyotaka musawada huo uondolewe ili
kutoa muda wa kujadiliwa na wadau.
Katika
taarifa yake hiyo kwa Bunge Mh. Mwandosya amewataka wadau wa habari waendelee
kutoa ushauri juu ya muswada huo pamoja na kuchangia maoni zaidi ili kupata
muswada ulio bora zaidi.
Prof
Mwandosya amesema muswada huo utawasilishwa na kujadiliwa katika mkutano ujao
wa bunge ambao utakuwa ni wa bunge la kumi na moja chini ya serikali ya awamu
ya tano.
Uamuzi
huo wa serikali umekuja kutokana na muswada huo kuzusha mgogoro na wadau wa
tasnia ya habari baada ya kuonekana kutowashirikisha wadau wa habari moja kwa
moja lakini pia kuonekana inaminya uhuru wa wananchi kupata habari.
Wadau
mbalimbali wa habari wakiwemo chama cha wamiliki wa vyombo vya habari MOAT
wamekuwa wakilalamikia maudhui ya muswada huo kwa madai ya kuminya uhuru wa
vyombo vya habari pamoja na haki ya kupata taarifa kwa wananchi.
Katika
mahojiano na mwanachama wa MOAT ambaye ni mwanzilishi mwenza wa mtandao wa
Jamii Forums jana (Juni 25) kupitia kipindi cha HOT MIX cha EATV Maxence Melo,
alisema kuwa endapo muswada huo ungepitishwa na kuwa sheria, basi tasnia nzima
ya habari ingekufa kwa kuwa umeweka njia ngumu ambazo hazitekelezeki katika
upatikana wa taarifa pamoja na mlolongo wa adhabu kali kwa wadau na waandishi
watakaokiuka sheria hiyo.
Naye
mwanasheria na mtafiti wa uchumi na biashara kutoka katika kituo cha sheria na
haki za binadamu Masud George kupitia kipindi hichohicho cha HOT MIX alisema
kuwa muswada huo ni hatari kwa uchumi wa nchi kwani shughuli nyingi za kiuchumi
zinategemea upatikanaji wa taarifa sahihi na kwa wakati.
Aliongeza pia kuwa, vyombo binafsi vya habari kama sehemu ya
wawekezaji katika sekta binafsi na chanzo muhimu cha ajira wanachangia kiasi
kikubwa cha uchumi wa nchi hivyo kuwadhoofisha ni kudhoofisha uchumi wa nchi
kiujumla.
0 comments:
Post a Comment