Najuta Kuvaa Nguo iliyoonesha Makalio Yangu – Faiza
01:28 by Kwetuhouse Media
Nguo aliyoivaa usiku wa June 13 kwenye tuzo za muziki za Kilimanjaro kwa nia ya kutoka kitofauti, imegeuka kuwa zimwi linalomtesa kiasi cha kumfanya apokonywe mtoto wake kwa amri ya mahakama na mzazi mwenzake, mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu. Faiza Ally anajuta!
“Siwezi kurudia kosa, nitakuwa makini zaidi katika mavazi yangu,” Faiza aliliambia gazeti la Mwananchi ambalo alienda kwenye ofisi zake kuelezea anavyojutia uamuzi huo uliomgharimu.
“Wasanii wengi ni wabunifu na hufanya mambo kwa nia ya kufurahisha mashabiki kama ambavyo amekuwa akifanya Joti kuvaa nguo za kike na kupaka rangi ya mdomo, hivyo mavazi yangu yalikuwa na lengo la kutoka tofauti mbele za mashabiki wangu, lakini kwa yaliyonikuta hasa kwenye vazi la Kili niliomba msamaha kwa jamii na bado naomba wanisamehe,” alisema Faiza huku akidaiwa kububujikwa na machozi.
“Hakika nimejikuta kwenye wakati mgumu na sivyo ambavyo baadhi ya watu wanafikiri. Hali hiyo ilinitokea nikiwa kule kule kwenye Kilimanjaro Music Award tena baada ya kubaini picha zinazoonyesha makalio yangu zimewekwa kwenye mitandao. Niliamua kuondoka haraka katika eneo hilo, kabla ya muda niliyokusudia,” aliliambia Mwananchi.
“Ingawa nimezoea kuvaa nguo fupi lakini sikupanga kuonyesha makalio, bahati mbaya ni kwamba ile nguo nilipoivaa awali kabla ya kuondoka nyumbani ilikuwa imekaa vyema. Nafikiri baada ya kukaa kwenye gari ilifumuka bila mimi kujua, hadi nafika ukumbini na kuingia pale kwenye zulia jekundu natembea kumbe huko nyuma mapaparazi wanapiga picha. Hakuna hata aliyenishtua. Napenda kuweka wazi naumizwa na watu ambao wanaendelea kusambaza hizo picha za makalio, watambue tu leo imenifika mimi lakini siku nyingine itawafika na wao maana sisi sote ni binadamu, tunafanya makosa kwa nyakati tofauti.”
“Namshukuru Mungu nimeweza kuhimili hali hii kwa kiasi fulani, maana naamini mtu mwingine angeweza hata kuamua kuwa mlevi au kuwa mbaya lakini nashukuru nina uamuzi wa kubadilika, nampenda mwanangu sitaki kuwa mbali naye.
0 comments:
Post a Comment