Msafara mpya wa meli
zilizowabeba wanaharakati wanaowaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina
umeelekea katika eneo la Ukanda wa Ghaza katika juhudi za kuvunja mzingiro wa
kidhulma uliowekwa na Israel dhidi ya wakaazi wa Kipalestina wa eneo hilo.
Moja ya meli
zijulikanazo kwa jina la Marianne of Gothenburg tayari imeondoka katika mji wa
Palermo nchini Italia. Msafara huo wa wanaharakati uliaanza safari yao kuelekea
Ghaza wakitokea Sweden mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu.
Msafara huo unaoelekea
Ukanda wa Ghaza unatazamia kujiunga na meli nyingine ambazo ziko njiani
kuelekea Ukanda wa Ghaza. Meli hizo ambazo zimebeba idadi ndogo ya suhula za
kitiba na misaada mingineyo zinatarajia kuwasili Ukanda wa Ghaza mwishoni wa
mwezi huu.
Meli kwa jina la Marianne of Gothenburg
imebeba wanaharakati kutoka Sweden, Canada, Norway pamoja na bi Ana Maria
Miranda Paza mwakilishi katika bunge la Ulaya kutoka Uhispania. Naye mbunge wa
Israel mwenye asili ya Kiarabu Basel Ghattas amesema kuwa atajiunga na
wanaharakati hao.
0 comments:
Post a Comment