Matumizi ya mitandao ya
kijamii kama Facebook, Twitter, Instagram ni kitu ambacho kimeshika chati sana
kwa sasa duniani, vijana wameonekana kuwa waathirika wakubwa wa matumizi ya
mitandao hii.
Kijana Little Wang
ambaye umri wake ni miaka 19 huko China aliona njia pekee ya kukomesha tabia
yake ya kupenda kutumia laptop na simu kuingia mtandaoni ni kujikata mkono
wake, alipoona hali haimwendei sawa aliita taxi impeleke
Hospitali ambapo hakuna aliyejua kinachoendelea nyumbani kwao, aliacha ujumbe
kwamba ametoka kwenda Hospitali na angerudi muda mfupi baadaye.
Madaktari walimfanyia
operation kuunga mkono huo huku wakiwa na matumaini kwamba baadae utaweza
kufanya kazi kama ilivyokuwa mara ya kwanza kabla hajaukata.
Mama yake Little
alisononeshwa na kitendo hiki na kusema hakutegemea mtoto wake angeweza
kujifanyia ukatili wa aina hii.
0 comments:
Post a Comment