13:15 by Kwetuhouse Media
Diamond Platnumz sasa ni ‘hotcake’ kiasi cha
kuwafanya wasanii wengi wa Afrika kutamani kufanya naye collabo, lakini kwa
uamuzi mpya alioupitisha wasanii wa Nigeria ambao hawajafanikiwa kufanya nae
wataikosa nafasi hiyo.
Platnumz ambaye Jumamosi iliyopita pamoja na msanii wa Afrika Kusini, Donald
wameshoot video ya collabo yao mpya, amesema kwa sasa amefunga milango ya
kupokea collabo za wasanii wa Nigeria. Hii inamaanisha zile collabo za wasanii
wanaomuomba yeye afanye nao.
“Sababu ya kusimamisha kwa sasa isiwe too much too much “ amesema Diamond
kupitia 255 ya Clouds Fm. “ kwa sababu mwanzo tulikuwa tunafanya collabo na
watu kwa sababu ya kutafuta tobo la kuingia Nigeria,tumeishaingia vizuri
Nigeria tunakubalika tunafahamika na nyimbo zetu zinafanya vizuri hata tukitoa
nyimbo ambazo tunatoa wenyewe tu zinahit, mfano kama Nasema Nawe navyokwambia
sasa hivi inafanya vizuri Nigeria, so inakuwa haina maana kila mtu
akushirikishe shirikishe unakuwa hauna umuhimu, zimebaki tu baadhi ya collabo
za ambazo za wasanii wanaofanya vizuri zitatoka baadae lakini sio kwa sasa hivi
kwani tumezisimamisha, kwani tumekuwa tukiombwa sana sana sana na wasanii wa
Kinigeria kufanya collabo tumesimamisha.”
Diamond ameongeza kuwa collabo ya mwisho kutoka Nigeria ni ile ya Kcee na yeye
iliyotoka hivi karibuni, ambayo wanatarajia kuifanyia video nchini Afrika
Kusini.
“katika nyimbo ambazo tumeshirikishwa itakuwa ya mwisho hii tumefanya na Kcee
kwa sasa ambayo kuanzia kesho tunaanza kushoot video yake ambayo inafanyika
hapa hapa South Africa, ilitakiwa tushoot Mozambique lakini kwa sababu nina
issue za kifamilia hapa South Africa imeshindikana kwenda Mozambique imebidi
nimwambie inabidi tushoot hapa hapa.”
Hata hivyo Diamond amesema miongoni mwa wasanii wengine wa Afrika ambao wametuma
maombi ya kufanya naye collabo ni pamoja na Ferré Gola pamoja na kundi la Too
Fan la Togo.
0 comments:
Post a Comment