Chama cha Mapinduzi
(CCM) Zanzibar kimesema kitendo cha Mawaziri na wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi wa Chama cha Wananchi(CUF) kususia kikao halali cha Baraza la
Wawakilishi kinaonesha wazi dhamira ya Chama hicho ya kutokuwa tayari kuendelea
na mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kutokana na kwenda kinyume na Katiba
ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Akizungumza na waandishi wa habari, katika Ofisi kuu ya Chama hichi iliyopo Kisiwandui, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai amesema Chama cha CUF kinaelewa wazi kuwa lengo la kikao cha bajeti ni kujadili mapato na matumizi ya Serikali ambayo hutumika kufanikisha shughuli za Kiserikali ikiwemo miradi ya maendeleo na matumizi ya kila siku.
Vuai amesema hoja ya wajumbe wa CUF ya kususia kikao hicho kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linaloendelea katika Wilaya ya Maghrib, kisiwani Unguja, haina mashiko na hawakuwatendea haki wananchi waliowachagua kwa ajili ya kuwatumikia.
Naibu Katibu Mkuu huyo amesema hoja hiyo ya CUF ni njama iliyoandaliwa kwa makusudi kwa lengo la kuhahakikisha wanachama wa CCM katika kisiwa cha Unguja, hawapati fursa ya kuandikishwa katika daftari hilo.
Hata hivyo, Vuai amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein kutokana na uongozi wake imara ambao umesaidia kuwaunganisha wazanzibari sambamba na kuisimamia vyema katiba ya Zanzibar bila ya kumbagua mtu yoyote kwa tofauti za kisiasa, kidini na kikabila.

0 comments:
Post a Comment