CCM Zanzibar yaionya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)
03:50 by Kwetuhouse Media
Chama cha Mapinduzi kimeitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (NEC) pamoja na serikali kupitia vyombo vya dola kuhakikisha uchaguzi mkuu ujao hautawaliwi na vitendo vya vurugu
Serikali imeombwa kuimarisha ulizni katika vituo vya kupiga kura na maeneo yote ya nchi, hasa baada ya kuripotiwa matukio ya uvunjifu wa amani wakati wa zoezi la uandikishaji wapiga kura wapya kwenye daftari la kudumu.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwera kichama Yussuf Mohammed, amesema lazima tume na vyombo vya dola vijipange vyema kuhakikisha uchaguzi huo unakuwwa huru na haki.
Amesema vitendo vya uvunjfiu wa amani vilivyojitokeza, vinapaswa kuizindua serikali juu ya wajibu w kuzidisha ulinzi ili kuiepushe Zanzibar na maafa yanayoweza kujitokeza wakati wa uchaguzi mkuu wa mwezi wa oktoba.
Aidha amesema iko haja kwa vyama vyote vya siasa nchini kuwataka wanachama wao kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuharibu uchaguzi na kufanya nchi kutotawalika.
Amesema iwapo chama au mgombea anahisi amenyimwa haki yake, wafuate sheria zilizowekwa kuwasilisha malalamiko yao kwenye vyombo husika badala ya kuanzisha vurugu.
0 comments:
Post a Comment