TANZANIA
imetupwa nje ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya sare
ya 1-1 jioni ya leo Uwanja wa Nakivubo, Kampala, Uganda.
Matokeo
hayo yanamaanisha, Stars imetolewa kwa kipigo cha jumla cha mabao 4-1, baada ya
awali kufungwa 3-0 katika mchezo wa kwanza wa Raundi hiyo ya kwanza visiwani
Zanzibar wiki mbili zilizopita.
Dakika
45 za kwanza zilimalizika kukiwa hakuna timu iliyopata bao na kipindi cha pili
na kipindi cha pili, John Bocco ‘Adebayor’ alianza kuifungia Tanzania kwa
penalti dakika ya 53 kwa penalti.
Kikosi
cha Taifa Stars kilichotoa sare ya 1-1 na Uganda leo Kampala
Penalti
hiyo ilitolewa baada ya beki wa Uganda kuunawa mpira uliopigwa na mshambuliaji
wa Tanzania, Rashid Mandawa.
Uganda
walifanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 82, kupitia kwa Kizito Hezron
na wanasonga mbele katika mbio za CHAN ya mwakani nchini Rwanda.
Matokeo
haya ya sare baada ya vipigo vitano mfululizo kwa Stars yanakuja chini ya kocha
mpya, Charles Boniface Mkwasa kufuatia kufukuzwa kwa Mholanzi, Mart Nooij baada
ya kufungwa na Uganda 3-0 Zanzibar.
Kikosi
cha Uganda kilikuwa; James Alitho, Muzamiru Mutyaba, Brian Ochwo, Hassan Waswa,
Denis Oola, Faruk Miya, John Shemazi/Robert Sentongo, Bakaki Shafik, Tekkwo
Derick/Kizito Hezron/Kalanda Frank.
Tanzania;
Ally Mustafa ‘Barthez’, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji Mngwali, Nadir Haroub
‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Frank Domayo/Said
Ndemla, John Bocco, Rashidi Mandawa na Simoni Msuva/Ramadhani Singano ‘Messi’.
0 comments:
Post a Comment