NACTE yafuta usajili wa vyuo vitatu na Vyuo vingine 16 nchini vyashushwa hadhi.

13:36 by Kwetuhouse Media


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi NACTE limefuta usajili wa vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo 16 katika jitihada za baraza hilo kulinda ubora wa elimu nchini.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Adolf Rutayuga amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya vyuo hivyo kushindwa kurekebisha kasoro zilizoainishwa na Baraza hilo. Amesema kwa kutumia sheria ya Bunge sura namba 129 na kanuni ya Baraza ya usajili ya mwaka 2001 na zile za ithibati, mnamo Februari 20 mwaka huu, NACTE ilitoa notisi ya siku 30 kwa taasisi na vyuo vilivyokiuka taratibu na vile vyenye mapungufu ya usajili na ithibati kujitetea na kufanya marekebisho yaliyoainishwa, lakini baadhi ya vyuo hivyo vimeshindwa kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa NACTE, Vyuo vitatu vilivyofutiwa usajili na kuzuiwa kudahili wanafunzi wapya ni Dar es Salaam College of Clinic Medicine, Ndatele School of Medical Laboratory Sciences na Institute for Information Technology vyote vya jijini Dar es Salaam, ambapo vyuo 16 vilivyoshushwa hadhi vipo katika maeneo mbalimbali nchini

0 comments:

Post a Comment